Breaking News

SANLAM GENERAL INSURANCE YATOA ZAWADI YA GARI KWA WAKALA WAKE

Dar es salaam:
Kampuni ya Bima ya Sanlam General Insurance imezindua kampeni kabambe kwa mawakala wao ambapo washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Gari, Bodaboda na zingine nyingi kupitia program ya Vuna Point.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi huo Meneja masoko na maendeleo ya Biashara, Matawi na mawakala wa kampuni hiyo, Bwana  Charles Magori amesema lengo la kuanzishwa kwa tuzo hizo ni kutoa hamasa kwa mawakala wa kampuni hiyo pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wao.

"Lengo kubwa la kuanzishwa kwa Tuzo hiI ni kutambua mchango wa mawakala wetu sambamba na zitawasaidia kuongeza ufanisi na ubunifu zaidi katika kutoaji wa huduma zao hivyo kupelekea kukua kwa mtandao wa biashara zao" Alisema Bw. Magori.

Alisema kampuni hiyo ambayo ina mtandao mkubwa mawakala ambao wanapatikana katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma, na Mbagala, Zanzibar na pia wanataraji kufungua mkoani Morogoro.

Katika hatua nyingine Bw. Magori ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kujiunga kuwa wakala wa kampuni hiyo kujitokeza kwa wingi ambapo ameeleza kuwa wanachotakiwa kufanya ni kupiga simu kupitia namba 0800750236 na kusajiliwa kuwa wakala.

Kampuni ya Bima ya Sanlam General Insurance ina zaidi ya uzoefu wa miaka 40 ya utoaji wa huduma za bima na soko la bima nchini imekuwa ikitoa huduma za Bima za Watu na Bima za  biashara.
 

No comments