Breaking News

RAAWU YAWAPA MBINU ZA KUJIANDAA KUSTAAFU WATUMISHI WA MAKUMBUSHO YA TAIFA

Na Mwandishi Wetu Dar.
Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Ufundi Stadi, Habari na Ushauri (RAAWU) kimetoa ushauri na mbinu za kujiandaa na kustaafu mapema kwa watumishi wa Makumbusho ya Taifa, katika mkutano wa mwaka wa watumishi wa Makumbusho ya Taifa unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu wa RAAWU Joseph Shayo amesema kuwa, kuna umuhimu wa kuanza miradi ya kuongeza kipato wakiwa bado kazini.

"Unajiona kijana kwa sasa lakini itafika muda wa kustaafu hivyo ni muhimu kuanza kujiandaa kustaafu" alisema Bw Shayo.

Amesema kuwa wastaafu wengi huanza miradi baada ya kustaafu jambo ambalo linakuwa halina mafanikio hivyo kutofanya vizuri.

Shayo ameongeza kuwa, ni vema watumishi kuanza kupata uzoefu mapema kabla ya kustaafu.

Amewataka watumishi hao kufanyakazi kwa bidii na maarifa kwa manufaa ya Taasisi na taifa kwa ujumla.

Aidha, amewataka watumishi hao kujiunga na chama cha wafanyakazi ili waweze kuunganisha nguvu za kutetea haki za  wafanyakazi.




No comments