LATRA YAKUTANA NA WADAU KUCHUKUA MAONI JUU YA NAULI MPYA SGR
Baraza la ushauri wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA) imetoa mapendekezo ya Nauli za treni ya Mwendokasi (SGR) kwa Daraja la kawaida kutoka Dar es Salaam Hadi Morogoro kwa shilingi 24,794 kwa Mtu Mzima wakati kwa mtoto Mwenye umri wa miaka 4-12 anatarajiwa kulipa 12,397.
Akizungumza katika Mkutano uliowakutanisha Wadau wa Usafiri nchini jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Ardhini LATRA bwana Habibu Suluhu amesema kuwa kwa Daraja la Kati kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro gharama ya Nauli inatarajiwa kuwa shilingi 29,752 wakati kwa mtoto Mwenye umri wa miaka Kati miaka hiyo hiyo itakuwa nishilingi 14,876.
"Kwa upande wa Nauli ya kutoka jiji la Dar es Salaam Hadi Dodoma kwa Daraja la kawaida mtu Mzima anatarajiwa kulipa shilingi 59,494 wakati mtoto anatarajiwa kulipa shilingi 29,747". Alisema Bw Suluhu.
Aidha bwana Suluhu aliongeza kuwa Nauli kwa Daraja Kati kwa mtu mzima anatarajiwa kulipa shilingi 71,392 huku mtoto natarajiwa kulipa shilingi 35,696.
Awali Mkuu wa Wilaya wa ilala mheshimiwa Bwilaguzu lubigija akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Malala amesema Serikali ya awamu ya sita imelenga kuboresha Miundombinu ili kuweza kumrahisishia mwananchi.
"Katika kuhakikisha tunaboresha huduma za reli kesho tunatarajia kusaini mkataba wa Ujenzi wa reli kutoka kigoma Hadi Tabora". Alisema Mhe lubigija.
Aidha Lubigija aliongeza kuwa kutokana na usafiri huo kuwa ni muhimu nchini ameishauri taasisi hiyo isiridhie Nauli hizo mpaka watakapo fikia makubaliano ya wadau wa Usafiri nchini juu ya nauli hizo.
"Kila mmoja aliyepo hapa ajisikie na awe huru kutoa maoni yake kwa lengo la kupata mapendekezo bora". Alisema Mhe. lubigija.
No comments