Breaking News

LATRA MFUMO WA UPANGAJI NAULI UMEKAMILIKA, KUANZA KAZI JUNE 2023

Mkuu wa wilaya ya ilala Arch. Ng`wilabuzu Ludigija akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau kujadili mapendekezo ya matumizi ya Taxi mita kwenye taxi nchini.
Mkurugenzi udhibiti usafiri wa barabarani bwana Johansen kahatano akifafanua jambo mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau kujadili mapendekezo ya matumizi ya Taxi mita kwenye taxi nchini.

Dar es salaam:
Mamlaka ya udhibiti usafiri wa Ardhini (LATRA) imesema kabla ya kufika mwezi juni mwakani 2023 tayari mfumo wa Taxi mita utakuwa umeanza kutumika.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wadau kujadili mapendekezo ya matumizi ya Taxi mita kwenye taxi nchini mkuu wa wilaya ya ilala Arch. Ng`wilabuzu Ludigija amesema matumizi ya taxi mita itamwezesha abiria kutoa kiwango sahihi cha nauli pia mfumo huo utaongeza usalama na uhakika kwa abiria.

"Hivi sasa mfumo unaotumika Dereva anatoza nauli kadri anavyojisikia lakini kwa kutumia taxi mita itawezesha abiria kutoa kiwango cha nauli ambacho ni sahihi na haki",

"Mbali na kulipa nauli sahihi ya uendapo, abiria utakuwa umejiridhisha chombo unachopanda ni chombo ambacho kinatambuliwa na LATRA kwa mujibu wa sheria" Amesema Ludigija.

Kwa upande wake mkurugenzi udhibiti usafiri wa barabarani Johansen kahatano amesema mfumo unaotumika hivi sasa katika kutoza nauli kwa abiria wa Taxi sio mzuri na haulindi maslai ya mtumi wa huduma.

Kahatano ameongeza kuwa Taxi mita ni mfumo wa uwazi,ukweli na uhakika kwa pande zote mbili yaani Abiri na Dereva kwani kila mtu ataona kiwango halisi cha nauli kulingana na umbali wa sehemu husika.

Nae kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC), Leo Ngowi amesema Sasa malalamiko kati ya Abiria na Dereva Taxi yameanza kupatiwa mwarobani pia amesema kuna nchi 9 Afrika moja ikiwa ni ya Afrika mashariki ambayo ni Rwanda ambazo zinatumia mfumo wa Tax mita.

Aidha LATRA CCC imetoa mapendekezo matatu ambayo ni Taxi zote zifungwe Taxi mita baadaya mfumo kuanza kazi,kuwe na ukomo wa gari kufungwa taxi mita pia Elimu itolewe kwa Abiria ili wajue uwepo wa Taxi mita na jinsi ya kutumia mfumo huo mpya.

Mwenyekiti wa Shirikishi la Taxi Tanzania Ramadhani Ashiru ameiomba LATRA kufanyiakazi changamoto zilizopo  ikiwemo Taxi bubu, bodaboda na bajaji kufanyakazi kiholela ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Taxi mita zinaendana na mazingira yaliypo ya ubovu wa barabara na foleni.

No comments