KILO 1543 YA DAWA ZA KULEVYA ZATEKEZWA JIJINI DAR
Bi Veronica Matikila akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya kuhusu zoezi la kuteketeza dawa za kulevya lilifanyika wazo hill leo 21 decemba 2022 jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchni (DCEA)imefanya zoezi la kuteketeza madawa ya kulevya yenye jumla ya kilo 1543.
Akizungumza na wakati wa zoezi hilo mapema leo 21 desemba jijini Dar es salaam, Bi Veronica Matikila kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa DCEA Gerald Kusaya katika amesema zoezi hilo la uteketezaji madawa hayo ni la kawaida hufanyika mara baada ya mashauri ya dawa za kulevya kuwa yamekamilika mahakani,”
Alisema katika zoezi ambalo limefanyika mapema leo jumla ya kilo 569.25 ni heroine, wakati kilo 15.3 aina ya Cocaine pamoja na tani mbili za bangi na mirungi.
"Dawa za Kulevya zilizotekezwa leo zimetoka katika mahakama mbalimbali ikiwemo mahakama kuu kanda ya Dar es salaam,mahakama kuu Division ya uhujumu uchumi,mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa pwani pamoja na mahakama za wilaya".amesema Matikila.
Alisema alisistiza kuwa zoezi la uteketezaji madawa hayo ni la kawaida, hufanyika mara baada ya mashauri ya dawa za kulevya kuwa yamekamilika mahakani hivyo kwa mujibu wa sheria kulazimika kufanyika kwa zoezi hilo
Picha mbalimbali za zoezi la uteketezaji jumla ya kilo 1543 za madawa ya kulevya zoezi lililofanyika katika kiwanda cha wazo hill jijini Dar es salaam.
No comments