Breaking News

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA SEKTA YA KILIMO NCHINI

Na Timothy Marko
Serikali imeongeza Bajeti ya Sekta ya kilimo kutoka bilioni 294 hadi shilingi bilioni 900 kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/23 ilikuhakikisha Sekta hiyo inachochea uchumi wa nchi.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Waziri wa Viwanda Biashara Uwekezaji mheshimowa Ashatu kijaji amesema fedha hizo zinalenga kuboresha Sekta ya kilimo Cha umwagiliaji ikiwemo kujenga Miundombinu ya umwagiliaji.

"Tumeongeza fedha kwa ajili ya kutengezafursa nyingi kwenye kilimo ilikuchochea Ajira kwa Vijana waweze kujikita kwenye kilimo hasa Cha umwagiliaji". Alisema Waziri Viwanda na Biashara Ashatu kijaji.

Dk kijaji Alisema kuwa Nivyema wadau wa sekta hiyo ya kilimo kushiriki Ana ilikuweza kuleta Mapinduzi ya Sekta hiyo.

Alisema Sekta hiyo ambayo inachangia Asilimia 27 katika kuleta fedha za kigeni imelenga kuboresha kuongeza thamani kwa Bidhaa za kilimo ili kuweza kuzalisha Ajira na usalama wa Chakula nchini.

"Pamoja na Sekta hii kuchangia ukuwajiwa uchumi nchini lakini inakabiliwa na Uhabawa wa Masoko kwa bidhaa zinazozalishwa na Uelewamdogo wa wadau ikiwemo wakulima kuhusiana kilimo Biashara". Aliongeza Dk kijaji.

Dk.kijaji Alisisitiza kuwa Nivyema wakulima wakapewa Mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha ilikuweza kuboresha Sekta hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo Cha    Uwekezaji nchini (TIC) John Mnali amesema kuwakatika kuelekea uchumi wa Kati wa juu taasisi hiyo imelenga kuboresha Sekta ya Viwanda Kama ajenda Muhimu katika taifa.

Alisema ilikuweza kuboresha Sekta ya Uwekezaji lazima kuwajengea uwezo Watalamu wa ndani.

"Lazima tuhamasishe Wawekezaji kuja kuwekeza nchini ilikuweza kuleta ujuzi kwa Watalamu wa ndani na kuwa hamasisha kulipa Kodi ilikuongeza wigo mpana wa Kodi". Alisema Mnali.

No comments