ASILIMIA 93 YA KAYA ZIMEIKIWA NA KUHESABIWA
Na Timothy Marko
Kamishina wa Sensa na Makaazi Anna Makinda amesema kuwa Hadi kufikikia 29 Agosti Mwaka huu Kaya Asilimia 93.45 ya kaya zimefikiwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Kamishina wa sensa Anna Makinda amesema ameongeza siku Saba kuanzia Leo Hadi September 30 Mwakahuu wahakikishe waleambao hawajahesabiwa wanahesabiwa.
"Kaya ambazo hazijahesabiwa ni Asilimia 6.5natoa wito ambao hawajahesabiwa wahesabiwe kabla jioni ya leo."Alisema Kamishina Anna Makinda.
Makinda Alisema Endapo mwananchi hajahesabiwa anatakiwa kwenda kwenye Serikali ya Mtaa husika ilikutoa taarifazake.
Aliongeza kuwa Endapo mwananchi hajahesabiwa anatakiwa kupiga namba0753665491, 0764443873, 0626141515, 0784665404, 0656279424 namba hizi zitatumika Hadi sept 5 Mwaka huu.
Makinda Alisisitiza kuwa Mara baada ya kukamilkazoezi Hilo kutakuwa na sensa yamajengo ili kujiweza kujitathimi katika uchumi wa Kati.
Naye Mkurugenzi wa Takwimu Emilian Karugendo amesema Makarani wa sensa wanaendelea kulipwa na fedha zipo kwenye Halimashauri wanazozifanyiakazi.
Alisema Mwenyekiti wa Mtaa anayemtembeza karani ndiye anatakiwa kulipwa.
"Vishikwambi vilivyopotea vimekamatwa kwa Baadhi ya Mikoa". Alisema Emilian Karugendo.
No comments