Breaking News

MEYA KUMBILAMOTO UKIKUTWA HATA GESTI UTAHESABIWA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Chanika William Abas Mwila akisalimiana na Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto katika kongamano la Sensa kutoa elimu kwa Wananchi wa Mtaa wa YONGWE Kata ya Chanika kongamano hilo limeandaliwa na Fahari Tuamke Maendeleo.
Meya wa Halmadhauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza katika Kongamano la Sensa ya watu na Makazi lililoandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo,Chanika Mtaa wa YONGWE (Kushoto) Mwenyekiti wa CCM Chanika William Mwila
Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Bi. Neema Mchau akizungumza katika Kongamano la Sensa lililoandaliwa na Taasisi yake ya Fahari
Afisa Mtendaji wa Chanika Charles Kimario akitoa Elimu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa niaba ya Mratibu wa Sensa Wilaya ya Ilala Mtaa wa YONGWE Chanika katika Kongamano la Sensa lililoandaliwa na Fahari Tuamke Maendeleo  (katikati)Mwenyekiti wa CCM Chanika William Abas Mwila na Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto .
Wanafunzi wa Fahari Day Care Center wakiwa na Mabango ya kuhamasisha Sensa katika Kongamano la Sensa lililoandaliwa na Fahari Tuamke Maendeleo katika Viwanja vya YONGWE Chanika. (Picha zote na HERI SHAABAN)

Na HERI SHAABAN (ILALA )
MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto  amesema Wananchi wa Wilaya ya Ilala wote watahesabiwa mpaka GESTI .

Meya Kumbilamoto alitoa kauli hiyo katika Kongamano la Sensa Kata ya Chanika Mtaa wa YONGWE lililoandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo ambapo Taasisi hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali kwa kutaka watu wahesabiwe kwa Maendeleo ya Taifa .

"Wananchi wote wa  Wilaya ya Ilala kila mtu atahesabiwa mpaka GESTI wote watahesabiwa taarifa zao zote zitakuwa Siri  naomba niwatoe hofu Wananchi watakaokutwa gesti siku ya mkesha wa sensa Agosti 23/2022 " Alisema Kumbiloto

Meya Kumbilamoto alitoa wito kwa Wananchi Wilaya ya Ilala kukaa nyumbani siku ya sensa ya Watu na Makazi Ili Serikali iweze kutenga bajeti yake ya Maendeleo kwa Wananchi .

Alisema dhumuni la sensa ya Makazi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupanga bajeti yake ya huduma mbalimbali zikiwemo za kijamii Afya, maji, Miundombinu nishati hivyo lazima iwajue Wananchi wake huduma ziwafikie kwa wakati.

Akizungumzia Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo Kumbilamoto alisema Serikali inatambua juhudi za Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo inavyosaidia Serikali katika sekta ya elimu na huduma za kijamii hivyo itashirikiana nayo kwani ni wadau wakubwa wa elimu.

Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau, alisema Fahari inashughulikia masuala ya Vijana, WANAWAKE na MAZINGIRA ambapo wamekuwa wakipanda miti katika Zahanati ya Yongwe kwa ajili ya utunzaji MAZINGIRA  Ili kuisaidia Serikali kutunza vyanzo vya maji.

Mkurugenzi Neema alisema Fahari Tuamke Maendeleo pia inajishughulisha na kulea watoto Ili Wazazi waweze kukuza uchumi waweze kusaidia Rais kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda.

Afisa Mtendaji Chanika Charles Kimario, akizungumza kwa niaba Mratibu wa sensa Wilaya ya Ilala alisema katika Wilaya ya Ilala asilimia 100 taratibu zote zimekamilika Pamoja na makarani wa sensa kwa ajili ya siku ya Agosti 23/2022 ambapo Watu wote watakuwa nyumbani kwa ajili ya kuhesabiwa.

Mtendaji Charles Kimario alisema  makarani wa Sensa na wasimamizi wote wameshakura viapo Pamoja na kupewa Elimu ya kutosha kwa ajili ya siku hiyo.

Aidha alisema Watu ambao wataondoka kazini siku hiyo Wanatakiwa waache vitu vyao muhimu ikiwemo Vitamburisho vya TAIFA ,Mpiga kura ,Leseni ya udereva na Mita Namba ya kulipa majengo yao.

Mwenyekiti wa CCM Chanika William Abas Mwila alipongeza Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo kwa juhudi za kuisaidia Serikali katika sekta ya Elimu Pamoja na kutoa elimu ya sensa .

Mwenyekiti William Mwila alitaka Fahari wapande miti ya Mazingira katika Hospitali ya Nguvu kazi na Ofisi za Serikali zilizopo Chanika Ili waweze Kitunza Mazingira na vyanzo vya maji.

No comments