Breaking News

Waziri BASHUNGWA AANZA NA TARURA AKERWA NA MIKWARUZANO INAYOENDELEA

Na.Angela Msimbira TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa akerwa  vikali  na mikwaruzano inayoendelea  kwa watumishi wa  Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) hali ambayo inaharibu taswira  na muonekano wa Taasisi hiyo muhimu  kwa jamii.

Akiongea na Menejimenti na watumishi wa TARURA  leo, Mtumba Jijini Dodoma  Waziri Bashungwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia. Suluhu Hassani  anamategemeo makubwa  na  Taasisi hiyo ambayo ndio kiungo muhimu katika  kutatua kero za wananchi. 

“Nimeifahamu migogoro ya TARURA kupitia kwenye vyombo vya habari, mikwaruzano yenu ya ndani inaonesha uhalisia wa migogoro iliyopo, Jambo hili halijanipendeza, hivyo mnanilazimisha kwenye majukumu yangu  ya kwanza  niwamulike kiundani, kwa hilo siko tayari  kuwa na Taasisi ambayo  badala ya kunisaidia nimsaidie Rais  katika kutatua changamoto za wananchi, yenyewe inakuwa na migongano ya kila wakati kugombana  badala ya kukaa ndani na kujipanga ili  kuweza kutatua changamoto  za wananchi” amesema  Waziri Bashungwa.
Waziri Bashungwa amesema ataingalia  taasisi hiyo kwa jicho la karibu ili kuweza kuhakikisha inatimiza majukumu yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi, na kusisitiza kuwa hatasita kuwachukulia hatua watumishi au viongozi  wachache  wanaotaka kuirudisha nyuma taasisi hiyo.

Amesema kuwa  si maadili na  ni kinyume na utaratibu wa kutoa siri za Taasisi au za Serikali  zinatoka nje kinyume na utaratibu, kwenye hili TARURA mmeonyesha mfano mbaya  kwa kuwa hali ya mikwaruzano ndani ya menejimenti inakwanza utendaji kazi wa Taasisi hiyo
Amesema hatakuwa tayari kwa mtumishi yeyote anayekwamisha  dira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa sababu ya watu wachache  wanaotaka kurudisha nyuma  utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hii Muhimu kwa jamii.

Aidha, amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuhakikisha anafuatilia    na kuchambua  mgogoro huo  na kuwaasilisha taaarifa ili  kuchukua hatua stahiki

No comments