Breaking News

ROSE MHANDO AMSHUKURU MCH. RICHARD MWACHA

Timothy Marko
Msanii wa nyimbo za Injili Bi. Rose Mhando ameshukuru Mchungaji wa kanisa la Fresh Spring Fellowship (Ngome ya yesu Kristo), mchungaji Richard Mwacha Kwa kumzawadia Gari Aina ya Toyota Prius.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Bi. Rose Muhando amesema katika kipindi chote cha uimbaji wake miaka zaidi ya ishirini pamoja na kupitia vipindi vigumu lakini Mungu amemuheshimisha Mchungaji huyo kuwasaidia waimbaji ikiwemo yeye.

"Katika maisha ya uimbaji nimepitia majaribu mengi lakini kwa wachungaji tupo tayari kupokea maonyo, ushauri na tupo radhi kukemewa kwani tuna wahitaji  sana'". Alisema Rose Muhando.

Muhando amevishukuru Vyombo vya Habari vya ndani na nje ya nchi na wadau wengine ambao katika kipindi chote wamekuwa nguzo muhimu kukuza na kutangaza huduma yake ya Uimbaji na wote walichangia huduma hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Muimbaji huyo Bw. Emanuel Mabisa amesema Rose Muhando amekuwa akipendwa na kupata kibali katika huduma yake ya Uimbaji katika katika ukanda wa afika ya mashariki.

" Pamoja na changamoto mbalimbali ambazo amezipitia katika kipindi chote cha miaka zaidi ya ishirini ya utoaji wa huduma yake ya uimbaji Rose Mhando amekuwa moja ya watoa huduma wanaopendwa ndani na nje ya nchi hasa katika nchi kama Kenya, Rwanda na Burundi". Alisema Bw. Mabisa.
 

No comments