Breaking News

CCM DAR YATOA TAMKO ZITO MSAMAHA WA SPIKA NDUGAI

Chama cha mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Dar es Salam, kimesema  hatua ya Spika wa Bunge, mheshimiwa Job Ndugai imeonyesha ukomavu wake  kisiasa na kujutia hivyo inapaswa kusamehewa.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salam, Bi. Kate Kamba alisema  bada ya Spika Ndugai  kuomba radhi hakuna sababu ya kuendeleza marumbano juu ya suala hilo.

“Hatuna sababu ya kuendelea na marumbano ambayo yatazidi kutugawa. Umoja wa taifa letu ni mshikamano. Mshikamani  ni wamaana sana kuliko  haya mambo mengine,”alieleza Kate.

Alibainisha, mtikisiko wa sakata la Spika Ndugai  badala ya kuwagawa watanzania lakini uliwaweka pamoja zaidi.

“Mtikisiko huu  umechangia kuimarisha umoja wetu. Umeona watanzania  jinsi walivyo kuwa wa moja. Tunampongeza ameomba radhi kwa watanzania walio kwazika. Imeonyesha ukomavu wake kisiasa,”alisema.

Alisema matukio mengi  mengi yaliyotokea yamekuwa yakiwaweka watanzania pamoja na kwamba sakata la Ndugai lilikuwa fundisho.

“Tanzania tunao uhuru wa kuongea na kusahihishana. Ndugai alizungumzza  maoni yake na ilionekana anaipenda Tanzania. Sisi  ni wanadamu, tunapokoseana hata Mwenyezi Mungu usamehe,” alibainisha Kate.

 

No comments