Breaking News

MSUYA: MHE NDUNGAI TAYALI AMEPOTEZA UHALALI WA KUENDELEA KUONGOZA MUHIMILI WA BUNGE

Mwanaharakati Bw. Daud Msuya amelaani kauli ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. Job Ndungai aliyoitoa katika mkutano wake na wanahanari juu ya mwenendo wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza jijini Dar es salaam amesema kitendo kile sio cha kufanywa na kiongozi wa muhimili mkubwa hivyo pamoja na kuomba samahani lakini tayali ameshapoteza uhalali wa kuendelea kuongoza chombo hicho.

"Kauli aliyoitoa mhe Ndungai tayali inatakiwa awe ameshajiuzulu nafasi yake mara moja kwani kitendo kile tayali ameshapoteza uhalali wa kuendelea kuongoza muhimili huo". Alisema Msuya.

Amesema kauli ile ilikuwa imejikita katika kumkwamisha mhe rais sambamba na kuonyesha kuwa hatua zote ambazo anachukua kuwaletea maendeleo wananchi ni batili.

"kilichofanyika ni kutaka kumkwamisha mhe rais Samia hivyo mpaka sasa nashangaa anangoja nini kujiuzulu nafasi yake kama spika kwani tayali ameshapoteza uweredi wa kuendelea kuongoza muhimili huo"

Binafsi nitoe rai kwa wanasiasa na viongozi wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamepanga kufanyia hujuma za aina yoyote mhe rais Samia kuacha mara moja mipango hiyo kwani tayali anayo list ya viongozi hao kama awatajirekebisha nitawataja adharani kwa majina yao.

No comments