Breaking News

JESHI LA POLISI LINAWASHIKIRIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA ZA KUMUUA BARKE RASHID

Jeshi la Polisi Dar limewakamata watu 2 wanaodaiwa kula njama ya kumuua Barke Rashid (30) Januari 1, 2022 katika nyumba ya kulala wageni eneo la Tabata Segerea.

Mwanamke huyo ameuawa  baada ya mpenzi wake White kulipa Tsh Mil1.7 kwa Jonsiner Bounser ili kutekeleza mauaji. 

“Inadaiwa mtuhumiwa wa 1 alikodiwa na mtuhumiwa wa 2 kwa malipo ya Sh1.7 mil ili amtongoze na baadae aende kumuua mwanamke huyo kwa madai kuwa mtuhumiwa wa 2 alimgharamia sana na kumpangishia nyumba lakini ilidaiwa na mtuhumiwa wa 2 kuwa mwanamke huyo ana wanaume wengine.

Mtuhumiwa wa 1 amekiri kupewa  Mil 1.2  kwa nyakati tofauti kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo na kwamba alikuwa bado anadai laki5  kwa mtuhumiwa wa 2 kwa mauaji ya mwanamke huyo, uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa na watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo.

No comments