Breaking News

WAZIRI MWAMBE KUFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA TAIFA LA USHIRIKI WA WATANZANIA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI NA UWEKEZAJI

Waziri wa  nchi ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji mhe. Geoffrey Mwambe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la tatu la Taifa la ushiriki wa watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji litakalofanyia tarehe 13 na 14 desemba jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) Bi. Bein'g Issa alisema Washiriki watajadiliana namna bora ya kuwawezesha watanzania waweze kushiriki katika miradi ya kimkakati na uwekezaji hatimae kumiliki uchumi wao wenyewe kwa asilimia kubwa.

"Wajumbe wa kongamano watajadiliana  kushiriki wa watanzania kwenye miradi ya kimkakati na uwekezaji pamoja na changamoto wanazokutana nazo katika miradi hiyo ya kimkakati". Alisema Bi. Bein'g Issa

Alisema kongamano hilo pamoja na washiriki kujadiliana pia limelenga kujikita zaidi kutafuta namna bora na kuwatengenezea mazingira bora ya ushiriki wao katika miradi hiyo.

Amewataja wadau wa watakao shiriki kongamano hilo ni Wizara na Taasisi za serikali, wakuu wa mikoa na wilaya zilizopitwa na miradi hiyo, Sekta binafsi, Taasisi za kifedha na Wakandarasi.

Amewataja wengine kuwa ni Waratibu wa mikoa na wilaya, Taasisi za utafiti na Elimu, Wadau wa maendeleo na Asasi za kiraia.

Kongamano la mwaka huu limebeba kauli mbiu ya "Wezesha Ushiriki wa Watanzania" limeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi na Mamlaka ya Mkondo wa juu wa petrol (PURA).

No comments