Breaking News

POLEPOLE: NIMEITWA TCRA KWA KURUSHA MAUDHUI YANAYOPOTOSHA KUHUSU CORONA

Ayekuwa katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi CCM mhe. Humphrey Polepole amepokea wito kutoka kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania kkufatia kukiuka sheria ya maudhui ya mtandaoni kupitia kipindi  vyake vya Shule ya uongozi ambavyo amekuwa akifanya kupitia chanel yake ya televisioni ya mtandaoni.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mhe Polepole amsema amepokea Mashtaka yanayosema kupitia Kipindi chake cha Shule ya Uongozi, amerusha Maudhui yanayoweza kuchochea Watanzania kuweza kugomea Kampeni ya Kitaifa ya COVID19

"Kama viongozi wasiposali na kumtemea Mungu nchi yetu haiwezi kuendelea, tumtangulize Mungu mbele. Kuanzia diwani, mpaka mawaziri na kule juu tuwe watu wa maombi, kukumbushana ni muhimu, naona kama tunatakiwa tuishi maisha ya Kimungu hivi." - Humphrey Polepole

"Viongozi wanatakiwa wawe waadilifu na wanyenyekevu." - Humphrey Polepole.

"Nilisema kuhusu magonjwa, mfano ebola, kesi moja tu imewahi kupenya na ikafuatiliwa na sasa tuko salama. Yakaja haya magonjwa mengine maarufu hivi karibuni lakini sio kitu. Nikasema muwe makini hawa wahuni wa kimataifa ni wajanja." - Humphrey Polepole.

"Nilizungumza kuhusu songombingo la wamachinga, Mhe. Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana lakini wapo waliotekeleza vizuri wengine wamefanya vibaya mno, wameboronga, ukimkosoa DC au RC kuhusu hili wanasema umemkosoa Rais, nani kakwambia?" - Humphrey Polepole.

"Rais Samia Suluhu alitoa maelekezo mazuri sana kuhusu wamachinga, wapangeni vizuri, msiwazonge, msiwapige, msiwanyanyase.... mimi ni mwana-CCM bana, fitina kwangu ni mwiko. Nikasema mlivyotenda kwa machinga baadhi yenu mmekosea na nikatoa mifano." - Humphrey Polepole.

"Kwenye mgongano wa kimasilahi kuna aina tatu, masilahi ya Taifa, kundi au mtu mmoja mmoja, wanaanza na masilani ya mtu mmoja, kisha kundi na baadaye Taifa, nikasema wanaopanga hivi ni wahuni." - Humphrey Polepole.

"Wahuni wanapenda masilahi binafsi kwanza, kazi yetu ni kuwadhibiti bila huruma wala kucheka nao. Yanatokea majitu tena viongozi na kusema mimi ni muhuni nimepenya, unaweza kutafakari namna gani kiongozi huyu yuko serious, huwezi kuwa kiongozi ukachekelea kuwa mhuni." -Polepole.

"Kule bungeni tunakutana mara chache, mfano kuna kipindi cha mwezi Machi hadi Julai, ina maana mimi niongee mara nne tu kwa mwaka kuhusu wahuni, unadhani inatosha, nitatumia fursa zozote za kusema ili kuwasema wahuni," - @hpolepole, Mbunge wa kuteuliwa.

"Kwa sasa nimeshaanza kufuatilia mambo kadhaa, watu wakizingua pahala ninatoka ninasema hapa umezingua nitaruka na wewe, nakulipua, si wanachelewa kuchukua hatua? - Humphrey Polepole.

"Sijasema Serikali haifanyi kazi, Serikali inafanya kazi nzuri sana lakini ni jukumu letu na kukumbushana. Unadhani kwa nini malaria haiishi na tumesoma mpaka madarasa tukayamaliza? Halafu tunasema tu lete net, hivyo viwanda wanatengeneza wapi?, vya msaada. - Humphrey Polepole.

"Nilieleza kuhusu uchambuzi wa matatizo, malaria haiishi Tanzania kwa sababu hatuchambui tatizo, unadhani ufumbuzi ni chandarua kwani ukitoka usiku kwenda haja ndogo mbu si wanaunga na wewe? tunafanya maamuzi ambayo hayajajengwa katika kutatua tatizo, hilo nalo tatizo." -Polepole

"Kuna kiwanda kipo hapa nchini kinatengeneza viuatilifu vya kuua mazalia ya mbu, nyie wanahabari waulizeni wamewahi kunnuua pale? Mtu analala kwenye chandarua mguu upo nje, mbu wanamng'ata, nauliza sisi tumekwenda shule tukasoma, hii ndio suluhisho kweli?" - Humphrey Polepole.

"Nilizungumza kuhusu deni la taifa, kuna watu wengine ni wabunge wakaibuka wanasema ooh deni limekuuwa kubwa, zito linamuelea mama. Nikatoka nikasema ukweli wasipotoshe, ni uongo. Si viongozi wote tupo kwa nini mwenzetu anapotosha na hatutoki kusema? kimya. -Humprhey Polepole.

"Sijui kwa nini viongozi wanaogopa kusema, sijui wanaogopa, kwa sababu deni linalosemwa viongozi wote walikuwepo, niweke sawa watu wasielewe tofauti. Kwa nini wenzetu msitoke mkasema, au mpaka watu wachanganyikiwe, penye ukweli lazima tuseme ukweli? - Humphrey Polepole.

"Juzi Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ndiye amekuwa mtu wa kwanza kutoka na kusema deni la Taifa ni himilivu, na yeye amejiongeza tu baada ya kuona kimya." - Humphrey Polepole.

"Sijazungumzia mtu, mbunge, mamlaka ya nchi wala mjomba wake mtu lakini baadhi ya viongozi wamechukia, kwa nini unaongea? Hivi imefika pahala tunaulizana kwa nini umeongea, Mungu amenipa mdomo unataka nifanye nini? Kuna kula na kuongea. - Humphrey Polepole.

"Nilipofanya Shule ya Uongozi nikapigiwa simu na watu wanaambiwa acha kwanza, nikauliza kwa nini? hakuna majibu. Nimefanya kazi na Mzee Mkapa, Kikwete, Magufuli na Mama Samia, hawa viongozi wangu wote hawajawahi kuniambia 'kaa kimya', nawashangaa wanaotaka ninyamaze." - Polepole.

"Mwalimu Nyerere alisema 'hoja ahipigwi rungu, inajibiwa kwa hoja bora zaidi', mimi ni mwana-CCM ninawaambia hapa kuna tatizo linarekebishika hivi, unasema kaa kimya, hilo ni jibu la hoja nilililoitoa." - Humphrey Polepole.

"Niliitwa kwenye chama kwa tuhuma, nilizijibu zote moja baada ya nyingine, siwezi kusema, chama kitakuja kuzungumza." - Humphrey Polepole.

"Nimeitwa TCRA, wanasema nimetoa maudhui ya kupotosha umma yanayoweza kuchochea Watanzania kugomea na kudhoofisha kampeni ya Kitaifa kujikinga na Corona. Hivi mimi nimeshawahi kuwaambia tudhoofishe kampeni ya kujikinga na corona? hawa wanataka kunichomeka hapa" -Humphrey Polepole

"Sijawahi kusema kwa nini sichanji, sasa tusisukumane nikafafanua kwa nini sikutaka kuchanja. Sasa nitakwenda TCRA kupeleka utetezi wangu nikaseme ukweli maana tunatafutana kwenye korido la corona." - Humphrey Polepole.

"Hii hoja ya wamachinga nasema kweli mmeonea watu, halafu mtu anasema kaa kimya, kumbe jukumu la mbunge ni nini? Sauti ya watu ni ipi? Hii kaa kimya nimehangaika nayo sana, nimefanya tu kiubishi." - Humphrey Polepole.

"TCRA wanasema wamenipa leseni kwa ajili ya maudhui ya kipindi cha Papo kwa Hapo, wanahoji kwa nini ninafanya Shule ya Uongozi... hivi mimi nimekulipa milioni ile halafu unanipangia cha kuzungumza? naweza kuposti familia yangu au mbwa wangu, utaniuliza?" - Humphrey Polepole.

"Kuhusu corona kuna ubishi wa kidunia, kila mtu ana upande wake, na mimi niweke wazi nipo kwenye ubishi huo. Mpaka Yesu atarudi tunaendelea na ubishi," Humphrey Polepole.

"Suala la machinga wanasema nimesema uongo, tena kwenye hilo nitasema na mengine ambayo sikutaka kusema, nina ushahidi, nimepeleka watafiti wilaya zote za Dar es Salaam, mtu amehamishwa na kupelekwa kwenye karo la choo, hivi Mhe. Rais aliwatuma hivyo?"-Humphrey Polepole.

"Kuna watu wanasema Polpole anajitoa CCM anakwenda kuanzisha chama chake, nataka niwaambie niliingia CCm kwa hiari mwaka 2000 nikapiga kura kwa mara ya kwanza, sitatoka CCM kwa hiari. Kama ninatoka CCM washike wanitupe nje, bado tupo sana hapa." - Polepole.


Mbunge wa Kuteuliwa (CCM),Humphrey Polepole amesema amepokea Mashtaka ya TCRA yanayosema kupitia Kipindi chake cha Shule ya Uongozi, amerusha Maudhui yanayopotosha Umma na yanayoweza kuchochea Watanzania kuweza kugomea Kampeni ya Kitaifa ya COVID19

Akizungumza leo amesema, "Hivi mimi nimewahi kuwaambia ninyi tudhoofishe Kampeni ya Corona? Wapi niliwaambia kwa maana hiyo?"

Amesema kwasababu amepewa nafasi ya kujibu, atapelekea Utetezi wake aliodai unajitosheleza.

No comments