Breaking News

WAZIRI MWAMBE AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA LOCAL CONTENT AWATAKA WASHIRIKI KUJADILIANA NA KUZIPATIA UFUMBUZI CHANGAMOTO ZILIZOPO

Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu-Uwekezaji mheshimiwa Geoffrey Mwambe akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la 3 la Local Content linalofanyika kwa siku mbili (13 na 14, Desemba 2021) katika Ukumbi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu ya Dar es Salaam.
Katibu mtendaji wa NEEC, Bi. Beng'i Issa akizunguza katika ufunguzi wa Kongamano la 3 la Local Content linalofanyika kwa siku mbili (13 na 14, Desemba 2021) katika Ukumbi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu ya Dar es Salaam.
Mtaalam wa tafiti kutoka taasisi ya Uongozi, Bw. Ramadhani Jambo akiwasilisha mada katika Kongamano la 3 la Local Content linalofanyika kwa siku mbili (13 na 14, Desemba 2021) katika Ukumbi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu ya Dar es Salaam.

Dar es Salaam:
Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu-Uwekezaji mheshimiwa Geoffrey Mwambe azitaka taasisi za serikali, sekta binafsi kujadiliana na kupata suluhu ya changamoto mbalimbali zinazokwamisha dhana ya ushiriki wa wazawa katika miradi ya kimkakati na uwekezaji nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la tatu la Local Content katika ukumbi wa maktaba mpya UDSM jijini Dar es salaam mhe. Mwambe amesema serikali utaendelea pia kushirikiana na wadau pamoja na kuweka mazingira rafiki kuwezesha wazawa kushiriki katika miradi hiyo.

"Nitoe wito kwa taasisi za serikali, sekta binafsi kujadiliana na kupata suluhu ya changamoto mbalimbali zinazokwamisha dhana ya ushiriki wa wazawa katika miradi ya kimkakati na uwekezaji inayoendelea nchini". Alisema Mhe. Mwambe

Mhe. Mwambe pia amewataka waandaji wa kongamano hilo kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wamiliki wa kampuni, mabenki, Sekta binafsi na wanafunzi  kutoka vyuo vikuu kuweza kujadili pamoja masuala ya local content jambo litakalo wasaidia kuwajengea uwezo wanafunzi kuweza kujiajiri na kuondokana na dhana ya kuajiriwa.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji kiuchumi (NEEC), Bi.  Beng'i Issa amesema lengo kubwa la kuandaa kongamano hilo ni kuwakutabisha watanzania kujadiliana na kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo hili kuwezesha  ushiriki wao katika fursa za kukuza uchumi jumuishi pamoja na kushiriki katika miradi mbalimbali ya Kimkakati na utekelezaji wake .

Alisema utekelezaji wa Local Content nchini Tanzania umelenga katika kutoa ajira kwa watanzania, zabuni katika kampuni za kitanzania ikiwemo bidhaa wanazozalisha, mafunzo na uanzishwaji wa Teknolojia pamoja na kuinua mfumo wa miradi.

Naye, Mkurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dr Frederick Ringo amesema kuwa, kwa kutambua mahitaji na  changamoto wanazopitia wajasiriamali wa Tanzania, kupitia dhana ya local content Benki hiyo imekuja na suluhu ya changamoto zao.

Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu-Uwekezaji mheshimiwa Geoffrey Mwambe akikabidhi Tuzo kwa washindi na wadhamini mbalimbali wa Kongamano la 3 la Local Content linalofanyika kwa siku mbili (13 na 14, Desemba 2021) katika Ukumbi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu ya Dar es Salaam.





Wadau mbalimbali wakifatilia mada zinazowasilishwa  katika Kongamano la 3 la Local Content linalofanyika kwa siku mbili (13 na 14, Desemba 2021) katika Ukumbi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu ya Dar es Salaam.

Picha ya pamoja Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu-Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe aliwa na kamati ya maandalizi ya Kongamano la 3 la Local Content linalofanyika kwa siku mbili (13 na 14, Desemba 2021) katika Ukumbi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu ya Dar es Salaam

No comments