Breaking News

WAZIRI MAKAMBA ARIDHISHWA NA UZALISHAJI WA KIWANDA WA AFRICA CAB

Na: Timothy Marko
Serikali imewataka wazalishaji wa bidhaa na vifaa vya umeme nchini kuzingatia kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Akizungumza katika kiwanda kinachozalisha bidhaa za umeme cha Africa Cab, jijini Dar es Salaam Waziri wa nishati, Mhe. January Makamba amesema Serikali tayali inatekeleza mpango wa kusambaza umeme vijijini ambapo jumla ya vitongoji 64000 Kati ya vitongoji 27000 ndivyo vyenye umeme.

"Kilometa 12,022 tayali zimefikiwa huku lengo likiwa ni kufikia kilometa 340000 za nyaya zinatakiwa kuwezehsa kuwafikia  watumiaji milioni tatu". Alisema Waziri Makamba.

Makamba alisema katika kufikia vijiji vyenye umeme wa uhakika ni lazima wazalishaji wa vifaa vya umeme kuzingatia uzalishaji wa bidhaa zenye Ubora.

Aliongeza Duniani kote hivi karibuni kumekuwa  na upungufu wa nyaya za alminiam hivyo alikitaka kiwanda hicho kuzalisha bidhaa hizo.

Naye afisa masoko wa kampuni ya Africab, Bw. David Tarimo ameiomba Serikali kuwaunga mkono kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndan kwa lengo la kukuza soko la bidhaa zao.

"Tunaiomba serikali kuendelea kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa na viwaanda vya ndani kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuvifanya kuweza kuzalisha zaidi bidhaa bora pamoja na kuongeza wingo wa kutoa ajira''. Alisema Tarimo.


 

No comments