Breaking News

NAIBU WAZIRI GENKUU MGENI RASMI UTOAJI WA TUZO ZA WAOGELEAJI JIJINI DAR

Timothy Marko
Naibu waziri  wa sanaa na Michezo Mhe. Pauline Genkuu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji Tunzo za Mashindano ya kuogelea zitazofanyika Desember 19 katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar essalaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam  Mkurugenzi wa Kampuni ya Champion Rise, Bi. Amina Mfaume amesema lengo la tuzo hizo ni kuongeza hamasa za mchezo wa kuogelea kwa wachezaji na wadau wa mchezo huo.

Alisema jumla ya washiriki 160 watashiriki katika siku hiyo ya kutoaji tuzo ambapo washiriki watachuana katika vipengele mbalimbali ikiwemo kipengele cha Muogeleaji wa mwaka, Muogeleaji Chipukizi  wa mwaka na Meneja wa Club wa mwaka. 
Mapema Mkurugenzi wa  masoko wa Kampuni hiyo Ally Nchahaga, amesema viingilio katika sherehe hizo ni shill laki moja kwa mtu mmoja, shilingu mill 1.5 kwa meza na shilingu mill moja kwa VIP huku akiwataka wadau wa chezo wa kuogelea kujitokeza kwa wingi.

"Nitoe wito kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa kuogelea, makampuni na vilabu kujitokeza kwa wingi katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo ili kuheshimisha mchezo wa kuogelea hapa nchi

No comments