Breaking News

WANAKIJIJI CHA NJINJO MKOANI LINDI WAMWOMBA RAIS SAMIA KUINGILIA KATI MGOGORO KATI YAO NA VIONGOZI WA SERIKALI

Na  Mwandishi Wetu Kilwa 
WANANCHI wa Kijiji Cha Njinjo Kata ya Njinjo Tarafa ya Njinjo wilaya kilwa mkoani Lindi wamemuomba rais Samia Suluhu Hassan kuingilia Kati mgogoro uliopo kati yao na uongozi wa serikali wilayani humo wa kutengeua maamuzi ya rais ya kujenga kutuo cha afya Njinjo na badala yake kuelekeza ujenzi huo kipindimbi. 

Wananchi hao wamesema kuwa rais Samia katika juhudi zake za kuimarisha afya za wananchi wake na katika kijiji hicho ambacho kinabeba kata alipeleka shilingi milioni 250 lakini cha kusikitisha viongozi wao wanahamisha kituo hicho na kupeleka kijiji cha kipindimbi. 

Akizungumza mbele ya wananchi wake katika mkutano ambao umefanyika kwenye eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Njinjo Muhidin Omar Amesema kuwa kumsingi wamesikitishwa sana juu ya maamuzi ya viongozi wao ngazi ya wilaya.

"katika hili mimi Kama kiongozi nimefika hadi Dodoma kwa lengo la kuonana na katibu Mkuu wa chama. Lakini tumhoji sana juu ya maamuzi haya ambayo yamefanyika haiwezi fedha umeletwa kwa ajili ya njinjo alafu watu kwa utashi wao wanapeleka kungine'"Amesema Omar
Amesema kuwa yeye Kama kiongozi anasimama na wananchi wake katika kile ambacho wanakidai na wanamuomba rais Samia kuingilia Kati sakata hilo ambalo linasababisha hasira kubwa dhidi ya wananchi na serikali yao

Pichani Wananchi wa kijiji cha Njinjo kata ya Njinjo wilayani Kilwa mkoa wa lindi wakiwa katika mkutano mkubwa uliowakutanisha waandishi wa habari ambapo waliitwa na uongozi wa serikali ya kijiji hicho kuzungumzia kero mbalimbali. 

No comments