Breaking News

MAOFISA 29, ASKARI 24 JESHI LA UHIFADHI - TFS WAVALISHWA VYEO VIPYA

MAOFISA 29 na askari 24 wa Uhifadhi katika Jeshi la Uhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) wamevalishwa vyeo vyao vipya kwa lengo la kuwawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwavisha vyeo hivyo iliyofanyika Kituo cha Mbegu mkoani Morogoro,Kamanda wa Kanda Kanda ya Mashariki , Caroline  Malundo amesema ni matakwa ya Jeshi la Uhifadhi askari kukamilika kwa mavazi na vyeo vyao rasmi.

"Kitendo hiki cha kuwavisha vyeo maaskari hawa ni  kwa niaba ya Kamishina wa Uhifadhi TFS Prof. Dos Santos Silayo ambaye ndiye alitakiwa hapa kwa ajili ya  kuwavisha lakini kutokana na majukumu mengine amenikaimisha nimemuwakilishe," amesema.
Amesisitiza katika Jeshi la Uhifadhi ni takwa mojawapo ni  askari kuwa katika vazi rasmi, kuwa katika cheo rasmi,cheo kinachomtambulisha yeye ni nani,kwa hiyo hawa askari na maofisa ambao jumla yao ni 53 wamevaa vyeo vyao wakiwa tayari sasa kwenda kutekeleza majukumu yao ya kijeshi.

 

No comments