Breaking News

LATRA: MADEREVA ZINGATIENI SHERIA NA KANUNI ZA USALAMA BARABARANI

Na Mwandishi wetu 
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka madereva wote nchini kuzingatia sheria na kanuni wanapotekeleza majukumu yao,

Kwa mujibu wa LATRA, Kanuni za Kudhibitisha Madereva na kusajili wahudumu wa magari ya biashara iliyotolewa katika gazeti la serikali Na. 81  toleo la mwaka 2020, madereva wote wa magari ya biashara wanatakiwa kujisajili ndani na LATRA na baadae kuthibitishwa.
Rai hiyo imekuja kufuatia hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya Tanzania ya kuondoa zuioa la shauri namba 87 ya mwaka 2019 lililofunguliwa na Umoja wa Madereva wa Mabasi Tanzania UWAMATA dhidi ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA/Mamlaka Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).


Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo Cha Mawasiliano  LATRA hukumu iliyosomwa na mahakama hiyo Disemba 16 mwaka huu,imetafsiri  sheria kuwa,madereva wa magari ya abiria pamoja na UWAMATA wapo chini ya LATRA.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, mahakama imewataka madereva kufuata sheria na kanuni wanapotekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa kufuatilia mwenendo wa Mabasi(VTS) lengo kuepusha ajali ambazo zinachangia vifo,ulemavu na uharibifu wa mali.

No comments