Breaking News

WAZIRI MKUMBO : TBS ANDAENI MPANGO WA KUWASAIDIA WAJASILIAMALI WADOGO KUFIKIA VIWANGO VYA UBORA

Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo ameitaka Shirika la Viwango Tanzania TBS kuandaa mpango maalum utakao wasaidia wajasiriamali wanaofanya ujasiriamali mdogo kwa lengo la kuwainua kupata viwango vya ubora.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo za ubora kitaifa kwa mwaka 2021/2022 jijini Dar es Salaam, amesema Tanzania ikiwa ni moja ya nchi wanachama imeitikia wito wa kuanzisha mashindano ya kitaifa nchini kuanzia mwaka 2020.

“Tunapozungumza ujasiriamali mdogo na mkubwa hapa nchini ni unazungumzia kundi kubwa zaidi ambalo ni zaidi ya asilimia 70 ya wananchi wetu hivyo nitoe wito kwa  TBS kukaa na wataalam wenu kuona namna ya kufanya kuwapa uzito wa kutosha,” Amesema Waziri Mkumbo.
Prof. Mkumbo pia ameziasa taasisi za umma na sekta binafsi kuhamasisha wazalishaji na watoa huduma kushiriki kwa wingi katika mashindano haya ili kupata washindi bora watakaowakilisha vyema Taifa katika mashindano ya tuzo za ubora SADC.

Naye Mkurugenzi wa TBS Dkt Athuman Ngenya amesema TBS inaendelea kutoa elimu hasa kwa kundi la wajasiriamali wadogo na kuhamasisha ushiriki zaidi katika mashindano ya mwaka huu.
Tuzo hizo zimegawanyika katika makundi matano kundi la kwanza ni Kampuni bora ya mwaka katika ukanda wa Kusini mwa afrika, Bidhaa bora ya mwaka, Huduma bora ya mwaka, Muuzaji bora wa bidhaa nje ya nchi na Tuzo binafsi ya mtu aliyechangia sana katika ubora.
Picha ya pamoja Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb)(wa tatu kutoka kulia)Mkurugenzi wa TBS Dkt. Athuman Y. Ngenya (wa nne kutoka kulia) na Kaimu Mkurugezi Mkuu wa ZBS wa pili kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za ubora za kitaifa kwa mwaka 2020.

No comments