Breaking News

WANACHAMA SABA WAGOMEA KUVULIWA UANACHAMA CUF

Wanachama Saba waliovuliwa uanachama wa chama cha wananchi (CUF) wamepiga kuvuliwa kwao uanachama wa chama hicho kwa madai kuwa hatua za kuwavua uanachama kutokukidhi matakwa ya katika ya chama hicho hivyo ni batili.

Wakizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake jijini Dar es salaam, Hamidu Bobali amesema Wanapinga maamuzi hayo yaliotolewa na kikao kikuu cha chama hicho kilichoketi 5 na 6 novemba Kuwa batili kufatia kukiuka ibara ya 11(6) ya katiba ya chama.

Ameseama maamuzi ya kikao hicho yanakosa uhalali kufatia kushindwa kutimiza ibara ya 11 (6) ya katiba ya chama hicho ambayo inaeleza wazi watuhumiwa kupewa nafasi ya kujitetea pia imekiuka azimio la kimataifa la haki za bianadamu pamoja na katiba ya nchi.

"Sisi bado wanachama halali na viongozi jasiri wa chama cha wananchi CUF kwa sababu maamuzi batili yaliyofanywa na kikao kikubwa cha juu kabisa cha chama kukiuka dhamira, itikadi na falsafa ya chama hicho" alisema Bobali.

Amesema maamuzi ya kikao hicho yanakosa uhalali kufatia pia kwa makusudi kupuuza matakwa ya ibara ya 115 (1)ya katiba ya chama ambayo inaelezea uhalali wa kura zinanzopigwa na wajumbe lazima zizidi nusu ya wajumbe walioshiriki.

Kwa upande wake Abduli Kambaya ambaye pia kikao hicho kiliadhimia kuvuliwa uanachama wake alisema kimsingi maamuzi ya kikao kwa mujibu wa katiba ya chama hicho yamekosa uhalali.

"Ibara ya 81 ya katiba ya chama inaeleza bayana wajumbe halali wanaotakiwa kushiriki katika kikao cha baraza kuu kilichotokea katika mkutano huo walikuwepo wajumbe ambao walishiki kikao hicho wakati walitakiwa kuwa walikwa tu" Alisema Kambaya.

Kambaya ameongeza kuwa rejea ibara ya 99 (2) katiba ya chama wajumbe halali wa kikao cha maadili cha chama kuelekeza sharti kuwepo na mwanasheria lakini kikao hicho hakikufanya hivyo.

Ametaja mengine kwa ni kukiukwa kwa kanuni ya 8.8 na kanuni ya jumuiya ya vijana ya chama hicho ambayo imeweka mashart ya hatua za kinidhamu kwa viongozi wakuu wa jumuiya.

"Kufatia mapungufu haya yaliyojitokeza katika kikao kikibwa cha maamuzi cha chama tumezamilia kuomba mwongozo wa kisheria juu ya baadhi ya vifungu ambavyo vimetumika kutuvua uanachama" Alisema Kambaya. 

No comments