Breaking News

CUF YAWAVUA UANACHAMA WANACHAMA 7 KWA TUHUMA ZA KUKIUJUMU CHAMA

Chama cha wananchi (CUF) kimewavua uanachama, wanachama wake 7 kati ya 14 ya waliokuwa na tuhuma za utovu wa nidhamu.

Akisoma maadhimio ya kikao cha baraza kuu la uongozi Taifa kilichokaa  5 na 6 novemba makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salam, 

Mkurugenzi wa habari, uenezi na mahusiano Umma, Mhandisi Mohammed Ngulangwa Amesema kikao hicho pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya nidhamu na maadili ya viongozi kulingana na mashtaka waliyokuwa wanakabiliwa nayo kikao kimeazimia kwa kauli moja kuwavua uanachama wanachama 7 na wengine kupewa honyo kali.

"Kwa mujibu wa katiba ya chama moja ya majukumu ya baraza kuu la uongozi la taifa ni kulinda na kue deleza heshima ya chama (ibara ya 8 (1)(e)"

Baraza baada ya kujiridhisha baadhi ya viongozi hao kula njama za kikuhujumu chama kwa kushirikiana na vingozi wengine wa kutoka vyama vingine ikiwepo kusajili chama kipya cha siasa hivyo kuazimia kwa kauli moja kuwavua uanachama.

Amewataja wanachama ambao wamevuliwa uanachama wa chama hicho kuwa na mhe. Hamida Huweishil, mhe. Dhifaa Bakari, mhe. Mtumwa Abdallah, mhe. Chande Jidawi.

Wengine ni mhe. Ali makame Issa, mhe. Mohamed Vuai Makame na mhe Adbul Juma Kambaya.

Aidha Mhandisi Mohammed Ngulangwa Amesema la kikao cha baraza la uongozi kwa kuzingatia uzito wa tuhuma na utetezi walioutoa kimetoa ovyo kali kwa baadhi ya wanachama na pia kusitishia  uanachama kwa mda wa miezi sita katika kipindi hicho watakuwa chini ya uangalizi wa chama.

Amewataja viongozi waliopewa onyo kali kwa maandishi kuwa ni mhe. Mussa haji Kombo, mhe. Yasin Mrotwa , mhe. Ali rashidi Abarania, mhe. Masoud Ali Said pamoja na Mhe. Hamidu bobali ambaye amepewaa kalipio kali na kuwekwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miezi sita.

Aidha Mhandisi Mohammed Ngulangwa Amewataka wanachama ambao awajaridhika na maamuzi hayo ya chama Wanaweza kukata rufaa ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe ya kuvulikwa kwao uanachama.

No comments