Breaking News

WAMACHINGA KUENDELEA KUFATA SHERIA NA TARATIBU ZILIZOTOLEWA NA SERIKALI

Wafanyabiashara wadogo wa kariakoo jijini Dar es salaam wamesema wataendelea kufata maelekezo na kuzingatia sheria na taratibu zilizotolewa na Serikali ili kufikia malengo kusudiwa kwa kumtoa Mmachinga toka kwenye biashara ndogo hadi biashara kubwa

Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa mtandao huu juu ya zoezi la kuwaamisha machinga jijini dar es Salaam Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Steven Lusinde amesema wao kama viongozi wa Machinga wamechukua maelekezo yaliyotolewa na Rais kuwaelimisha, kuwapanga na kuwaratibu watu wao.

Amesema Tukiwa kama viongozi wa wamachinga tayali tumeshatoa maomba menejimenti na Serikali tumehakikishiwa kuwa watafanyiwa kazi hivyo tutaendelea kuwa na ushirikiano ili kuondoa sintofahamu miongoni mwa wafanyabiashara hao

"Tulipata maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu septemba 10 mwaka huu namna ya kuendesha zoezi la kuwapanga vema wafanyabiashara wadogo kutoka maeneo yasiyo rasmi na kuwapeleka maeneo yaliyo rasmi," Alisema bw. Lusinde

Amesema kwa mujibu  maagizo waliopatiwa juu ya utaratibu huo tumebaini baadhi ya changamoto katika kitekeleza zoezi hilo ikiwemo uchache wa eneo ukilinganishwa na idadi halisi ya wafanyabiashara wanaotaraji kupelekwa katika maeneo hayo.

Aidha bw. Lusinde ameongeza kuwa chama cha wafanyabiashara wadogo (machinga) kipo katika hatua za mwisho za usajili wa taasisi yao, Hivyo kuiomba Serikali kuwa nao bega kwa bega katika majukumu mbalimbali ya kitaifa ya kibiashara kuwawezesha mikopo na kuwasaidia kupata uhalali kutambulika katika taasisi mbalimbali kama Bima za afya, Umeme na Maji.

No comments