Breaking News

LHRC, THRDC NA TAS WALAANI KUFUKULIWA KWA KABULI LA ALBINO MKOANI TANGA

Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kwa kushirikiana Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) na mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (THRDC) wamelaani tukio la kufukuliwa kwa kaburi la marehemu Heri Shekigenda aliyekuwa na ualbino na kuchukua polisi ya viungo vyake.

Akisoma tamko hilo jijini Dar es salaam, mkurugenzi wa LHRC, Adv. Anna Henga amesema marehemu Shekigenda alifariki kwa maradhi ya kansa ya ngozi July 4 na kuzikwa  7 July mwaka huu katika kijiji cha Tanda wilayani Lushoto mkoani Tanga.

"Kwa mwaka 2021 tukio hili ni la pili kuripotiwa ambapo mei 3 na 4 iliripotiwa mwili wa mtoto mwenye ualbino ulikutwa umekatwa mikono napenda kutoa wito kwa serikali ma jamii kushirikiana kwa pamoja kutokomeza matukio haya ma wahusika wachukuliwe hatua za kisheria" Alisema Adv. Henga.

Alisema tayali tukio limesharipotiwa katika kituo cha polisi Bumbuli kilichopo wilayan lushoto napenda kutoa rai kwa serikali na jeshi la polisi kuhakikisha kesi hii haitaishia katika ngazi ya upelelezo bali wahusika wote wasakwe na wafikishwe mahakamani.

"Matukio kama haya pamoja na kuvunja haki, utu na heshima ya binadamu pia ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 127 na 128 sheria ya kanuni za Adhabu sura ya 16 ya mwaka 2019" 

Nae katibu wa chama cha albino bw. Mussa Kabimba amesema  kuanza tema kwa matukio hayo nchini ni moja habari mbaya na ya kusikitisha hivyo kuliomba jeshi la polisi nchini kuhakikisha wanawatafuta wahusika wa tukio hilo.

"Chama tumesikitishwa na kuanza tena kwa kwa matukio haya ya mauaji ya watu wenye ualbino nchi jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina kuwabaini wahusika pamoja na kuhakikisha litokomeza matukio haya"

Kwa upande wake mwakilishi kutoka mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (THRDC), Bi. Perpetua Senkoro ameitaka jamii kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za zitakazo saidia kuwafichua wanaojihusisha na vitendo hivyo.

"Napenda kutoa wito kwa jamii kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua wahusika wa matukio hayo kufatia kuanza kushamili tena hivyo kuwatia hofu, wasiwasi na mashaka watu wenye ualbino nchini". Alisema bi. Senkoro.

No comments