USIKU WA TENZI ZA ROHONI UMERUDI TENA, KUFANYIKA OKTOBA 2021 DAR
Mpiga Saksafoni, Misericordias Mushi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akitambulisha usiku wa Tenzi utakaofanyika Ijumaa Oktoba 29,2021 katika kanisa la KKKT Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mpiga Saksafoni, Anta Simoni, Paustellah Mangilile na kulia ni Magreh Mushi.
Innocent Simon akipiga Saksafoni wakati wa kutambulisha usiku wa Tenzi za Rohoni kwaajili ya kusifu na kumwabudu Mungu kwa nyimbo, filimbi na vinubi siku ya Ijumaa ya Oktoba 29,2021 katika kanisa la KKKT Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Picha na Erasmus Kamugisha.
Paustellah Mangilile akizungumza na waandishi wa haari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 26,2021 wakati wa kutambulisha usiku wa Tenzi utakaofanyika Ijumaa ya Oktoba 29,2021 katika kanisa la KKKT Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
Dar es Salaam:
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 26, 2021, Mpiga Saksafoni, Misericordias Mushi amesema kuwa Ibada ya Usiku wa Tenzi za rohoni haitakuwa na kiingilio kiingilio ni Moyo wa utayari tuu.
Amesema kuwa Ibada hiyo itaanza saa tatu usiku mpaka Majogoo na waimbaji mbalimbali watakuwepo pamoja na wapiga saksafoni wanatuwepo mubashara.
Licha hayo Mushi amesema kuwa wataokuwepo ni pamoja na Anta Simon, Mwikiza Mwililu, Glory Akyoo, Dominic Mwakatobe, Moses Zamaywe, Lwitiko Mwagaya, Zephania Malambela na Mwalimu Fanuel.
Amesema kuwa lengo kuu la Ibada ya Tenzi za rohoni ni kumsifu Mungu kwa tenzi za Rohoni.
"Kizazi kilichopo wengi sana hawatumii Tenzi za rohoni wanatumia midundo ya kizazi kipya au midundo ya Kinaigeria, wanasahau nyimbo za tenzi ambazo ni nyimbo mhimu sana na zinaupako kama hizo nyimbo nyingine ." Amesema Mushi
Amesema wameona watumie nyimbo za Tenzi za Rohoni kusifu na kumwabudu Mungu kwani wameona matokeo halisi katika maisha ya kanisa namatokeo ya duniani.
Amesema watatumia Chombo aina ya Saksafoni kuimba, kusifu na Kuabudu kwa nyimbo za Tenzi za rohoni katika usiku wa Tenzi ambapo watakuwepo Vijana, watoto na rika zote kwajili ya kumsifu na kumwabudu Mungu.
Mushi amesema kuwa katika Ibada hiyo wapiga Saksafoni watapata nafasi ya kupiga mmoja mmoja na baadae watapiga saksafoni hizo kwa pamoja katika usiku huo wa Tenzi za Rohoni.
Katika ibada hiyo kutakuwa na kwaya ya Kanisa la KKKT Mbezi beach pamoja na waimbaji mmoja mmoja pamoja waimbaji binafsi.
Licha ya hayo Usiku huo wa Tenzi za Rohoni kutakuwa na Muda maalumu wa Kumshukuru Mungu kwa kutuvusha katika kipindi cha Ugonjwa wa Covid 19.
"Tutatenga muda maalumu wa Kumshukuru Mungu kwa kutupa uzima, kutuponya na hata kufika siku ya Oktoba 29, 2021 ambayo ni mwisho wa mwezi wa Oktoba, pia tutamwomba atupe nguvu ya kuendelea kumsifu na kumwabudu." Amesema Mushi.
Amesema kuwa usiku wa Tenzi utakuwa ni usiku wa kuwafundisha vijana na watu wote kuwa na uasilia wake (Originality) ikiwa ni moja ya Juhudi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suruhu Hassani kuwarudisha vijana na jamii kwa ujumla kuwa na maadili mema katika jamii.
Sisi kama watu wa dini tunasaidia vijana pia kurudi katika maadili yake na sio kuwaacha wapotee katika maadili yanayofaa.
Kwa Upande wake Magreth Mushi amemshukuru Mchungaji wa kanisa la KKKT usharika wa Pwani Mbezi Beach kutenga siku hiyo kwa ajili ya ibada ya Tenzi
No comments