Breaking News

Taasisi ya Wakati Wako Kusaka Vipaji Jijini Dar

KATIKA kukuza na kuibua vipaji kwa vijana wanaoishi familia masikini nchini,Taasisi ya wakati wako kwa sasa imeandaa programu maalumu  ya kuibua vipaji na kuwaendeleza kwa kuwafadhili masomo.

Akiongea jijini Dar es Salaam Katibu na mratibu wa program hiyo bw. Hassan Abdurahamani, alisema mashindano hayo yatahusisha sanaa ya uimbaji na kucheza.
 
Alisema vigezo vya vijana wanaohitajika katika mashindano hayo ni wenye vipaji na wasiojihusisha na makundi maovu.

"Juni 17 mwezi huu tutakuwa na tamasha ambalo tutatafuta vipaji vya vijana wanaoimba na kucheza,pia katika tamasha hilo tutawashindanisha warembo yaani kumtafuta miss na mista na wote wanaoihitaji sifa lazima awe kuanzia miaka 18 mpaka 27"alisema.

Alisema  milango tayari inekwisha kufunguliwa kwa vijana hao  kuanza kupeleka maombi yalipo makao makuu ya ofisi ya taasisi hiyo Amana Dar es Salaam .

Abdurahamani alisema, vijana wanao patikana katika mashindano hayo, watapata fursa ya kusafirishwa nje ya nchi kushiriki mashindano hayo makao makuu ya Taasisi ya  wakati wako kwa sasa nchini Afrika kusini.

"Vile vile tuna mpango wa kujenga shule kwaajili ya kuendelea kuibua vipaji kwa vijana hawa masikini, wote wanaoihitaji kushiriki nu bure waje kuchukua fomu ofisi zetu Amana na Tabata Aroma  Dar es Salaam"alisema.

Abdurahamani alisema, watakaokuwa na vipaji vya kuimba watafadhiliwa kurekodi bure  na kupewa zawadi mbali mbali  na kusomeshwa bure kwa wale wote wenye vipaji.

Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la EAGT Pugu  Dar es Salaam Cellestine Enock,  alisema vijana wengi wana vipaji  hivyo programu hiyo itawanua wengi.

Alisema wapo vijana wenye vipaji na wamekosa wakuwashika mkono hivyo hatua ya kuandaa tamasha kuibua vipaji vya vijana hao na kuviendeleza, ni jambo la kuigwa na taasisi zingine.

No comments