Breaking News

Rais wa TCCIA Awataka Wajasiliamali Kujikita Katika Matumizi Ya Teknolojia

Rais wa TCCIA, Bw. Paul Koyi akiongewa wakati akifunga warsha kwa wajasiliamali iliyoratibiwa na GIZ kuwajengea uwezo kufanya biashara zao kwa njia ya mtandao jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Chama cha Wafanyabiashara Nchini TCCIA imewataka wanawake wajasiliamari kupenda kutumia teknolojia ili kuwasaidia kufanya biashara zao kupitia mdandao nakuweza kukabiliana na ushindani wa masoko uliopo kwa sasa.

Rai hiyo ilitolewa na rais wa TCCIA, bw. Paul Koyi wakati akifunga mafunzo ya ujasiliamari mtandaoni ambapo wanachama wa Saccos ya wanawake Wajasiliamari nchini (TASWE) walikua wakifundishwa namna ya kufanya biasha zao kwa njia ya mtandao.


Mwenyekiti wa Saccos ya wanawake Wajasiliamari Tanzania (TASWE), Bi Anna Matinde akifafanua jambo wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiliamali kuhusu kufanya biashara kwa mtandao iliyoandaliwa na GIZ jijini Dar es salaam.

Awali mwenyekiti wa Saccos ya wanawake Wajasiliamari Tanzania Taswe Bi Anna Matinde alisema kuwa mafunzo hayo yamewashirikisha wajasiliamari wanawake wapatao mia moja nakwamba lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kufanya biashara kwa njia ya mtandoa.

Alisema mafunzo hayo yameanza juni mos na kumalizika juni 4 mwaka huu chini ya ufadhili wa shirika la Maendeleo la Ujerumani ( GIZ ) nakwamba yametolewa na kampuni ya Epvate and fortune international  Consulting iliyopo jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo bi.Rechel Damson ambaye anamiliki duka la dawa  la Tripple E huko Mbwen Beach amesema kwamba mafunzo hayo yamemsaidid kufahamu mambo mengi muhimu kwenye biashara ikiwemo namna ya kutunza kumbukumbu za fedha,kumeneji fedha hata inapokua kidogo, pamoja na kutafuta masoko ya kimataifa.

Rais wa TCCIA, bw. Paul Koyi akitembelea kujionea bidhaa zinazo zalishwa na wajasiliamali ambao wameshiriki mafunzo ya yalioratibiwa na GIZ juu ya kufanya biashara kwa njia ya mtandao jijini dar es salam.

Rais wa TCCIA, bw. Paul Koyi akitoa vyeti kwa washiriki mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiliamali kuu ya kufanya biashara kwa njia ya mtandao, Mafunzo hayo ambayo yameratibiwa na GIZ.
Mwenyekiti wa Saccos ya wanawake Wajasiliamari Tanzania (TASWE), Bi Anna Matinde akiwa katika picha ya pamoja na watoa mada katika warsha ya kiwajengea uwezo wajasiliamali kuhusu kufanya biashara kwa njia ya mtandao iliyoratibiwa na GIZ jijini Dar es salaam.

No comments