Breaking News

Mhe Hamad Rashid: Viongozi wa Vyama Vya Upinzani Kukutana Kabla ya Kumwona Rais

MWENYEKITI wa Chama cha Allience for Demoktatic Change (ADC) mhe. Hamad  Rashid  ameshauli viongozi wa vyama vya siasa nchini kupitia Baraza la Vyama vya siasa kukutana kwanza na kujenga maazimio ya pamoja kabla ya kwenda kukutana na Rais Samia Hassan Suluhu.

Akizungumza makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dat es salaam, Mwenyekiti chama hicho mhe. Hamad Rashid  alisema mkutano utawasaidia viongozi hao kuwa na ajenda muhimu za kitaifa.

"Ili kuwa na kauli ya pamoja kabla ya kwenda kuonama na mhe. Rais nashauri itapendeza kama tungekutana kwanza vingozi wa vyama vya siasa kukaa na kuzungumza kupata ajenda kuliko kwenda kila chama na hoja zake"Alisema mhe Hamad.

Mhe Hamad akitoa Msimamo wa chama cha ADC hicho katika ushiriki wa chamaa hicho katika chaguzi alisema chama cha  ADC dhamira yake ni kushika dola kuazia ngazi ya chini hadi taifa.

"Chama cha  ADC dhamira yake ni kushika dola kuazia ngazi ya chini hadi taifa hivyo hawawezi kususia uchaguzi  wowote na huku wakivitaka vyama vingine vya siasa kuachana na misimamo hiyo kwani haina afya kwenye medani ya kisiasa." Alisema 

Alisema chama kitashiriki katika uchaguzi wowote utakaokuja na hata ule uchaguzi mdogo wa  Jimbo la konde lililopo kisiwa cha Pemba Zanzibar  ambapo Jimbo hilo lipo wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo.

Kumekuwepo na malalamiko ya kukisema chama kwamba kinakwenda kinyume na misimamo ya vyama vingine ni kweli kwa sababu wao hawaamini katika kususia uchaguzi bali wanaamini katika kuwapa haki ya kidomokrasia Wananchi ili kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Pongezi Kwa kada wa Chama hicho Queen Sendiga

Katika hatua nyingine Chama cha ADC kimempongeza Rais  Samia Kwa kuweza kukiamini chama hicho na kuweza kumteua aliyekuwa Mgombea wa urais kupitia chama hicho Queen Sendiga kuwa Mkuu  mpya wa mkoa wa  Iringa nakwamba kamati ya utendaji ya chama hicho kimetoa baraka zote.

Ahmad alisema kwamba  kiongozi amepikwa vizuri ana uweledi wa kutosha ni makini nakwamba atamsaidia Rais Samia kutekeleza majukumu yake na wao kama chama watampa ushirikiano wa kutosha.

Kuhusu kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi sio tatizo kwani ndio chama kilichoshika dola kwahiyo wao hawajali hili nakwamba hata yeye Kwa mara kwaza aliteuliwa kuwa mbunge chini ya Serikali ya awamu ya tatu ya Benjamini mkapa .

Aliongeza kuwa hata katika serikali ya awamu ya saba chini ya Rais Dkt Ally Mohamed Shein alimteua kuwa Waziri katika Serikali yake hivyo kikubwa ni kutekeleza majukumu uliyoaminiwa na mamlaka husika.
Salamu za pole Kwa Rais Samia 

Kwa upande wake katibu Mkuu wa chama hicho Hassan Doyo Hassan alisema kwaniaba ya chama chake wanatoa pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan jKwa kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu  ya tano Dkt John Magufuli  ambaye alifariki Machi 17 Mwaka huu.

"Huu ni msiba mkubwa sana na wakihistoria kuwahi kutokea kwa taifa letu pendwa Kwa kuondokewa na kiongozi wa Nchi aliyemadarakani .sisi kama Adc tunasema pole sana Kwa msiba huu." Alisema 

Nakuongeza kwamba pia wanampongeza Kwa kuteuliwa kwake kuwa mwanamke wa kwanza katika ukanda wa afrika mashariki Kwa kushika nafasi ya uraia na kikubwa watanzania kumpa nguvu,moyo ili aendelee kuchapa kazi na pia wamempongeza Dkt  Philip Mpango kushika nafasi ya Makamu wa Rais .

Aidha bw. Doyo ameelezea kuhusu mwenyekiti wa Bodi na kamati ya utendaji ya chama hicho kimemtea Alhaji Shoka Hamis kushika nafasi aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo  Alhaj Ayub Mussa Kimangale kujiuzulu.

Pia katika hatua nyingine chama kimemtea bw. Twaha Said Mngatwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo .

Alisema baada ya kuonekana mwanga katika siasa chama kupitia kamati tendaji imeazimia kufanya ziara nchi nzima kukutana na viongozi na waliokuwa wagombea wa nafasi Kwa lengo la kurudisha uhai wa chama baada ya miezi sita tangu kumalizika Kwa uchaguzi mkuu wa 2020.

No comments