JATU Plc Yazindua Kampeni ya "Buku 5 Inatosha"
Kampuni ya Kilimo na Biashara ya (JATU PLC ) imezindua kampeni ya ununuzi wa hisa milioni moja na laki tano za kampuni hiyo zenye thamani ya shilingi bilioni saba na nusu (Bilioni 7.5) pamoja na utekelezaji wa mradi mpya wa kilimo cha umwagiliaji wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo Bw.Petter Isole wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo Kama "Buku 5 inatosha "ambapo inatarajia kuwanufaisha watanzania wengi ambao watanunua hisa za kampuni hiyo.
Bw. Isole alisema kuwa kiwango cha chini cha hisa za Jatu Plc ni shilingi elfu tano kwa hisa kumi, ambapo mteja inamfanya anakuwa sehemu ya umiliki wa kampuni nakwamba kiwango hicho kimewekwa kwa ajili ya kuwezesha watanzania waweze kumudu kununua hisa hizo.
Alisema kuwa kampuni hiyo imepata waraka wa idhini Kutoka serikalini kwa ajili ya kuuza hisa za kampuni ya Jatu Plc ili kuwezesha mtu yeyote anayetaka kununua hisa hizo aweze kunununua ili apate faida.
Akizungumzia mradi wa Kiteto Bw.Isole alisema kwamba mradi huo utakua na ukubwa wa hekari elfu tano ambapo kampuni hiyo imepanga kuwekeza miundombinu ya kisasa ya kilimo cha umwagiliaji nakwamba mazao mbalimbali yanatarajiwa kulimwa ikiwemo Mahindi.
Alisema kwamba mazao yaliyowekewa mkakati na kampuni hiyo kwa awamu ya kwanza ni mazao ya chakula ikiwemo Mahindi, Alizeti, Mchele, Maharage ambapo kwa awamu hii ya pili yameongezwa mazao mengine yakimkakati ambayo ni mazao ya matunda ikiwemo Kilimo cha mazao ya Maparachichi na Machungwa.
Aidha aliongeza kusema kuwa changamoto zinazoikumba kampuni hiyo iliyoanzishwa na wazawa ni pamoja na kukosekana kwa ardhi kwa ajili ya kilimo hivyo ameiomba serikali kuisaidia kuondoa changamoto hiyo.
Uzinduzi huo wa ununuzi mpya wa hisa za Jatu Plc umehudhuliwa na wanachama na mawakala wa kampuni hiyo kutoka sehemu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kupeana taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya miradi ya kilimo inayotekelezwa na kampuni hiyo.
No comments