Rais wa BOTSWANA kuwasili Kesho nchini Kwa Ziara Ya Siku Mbili
Rais wa Botswana Dr. Mokgweetis Masisi anawasili leo Nchini kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko wa rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan.
Akizingumzia ujio huo jijini Dar es salaam waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberatha Mulamula alisema kwamba ziara hiyo inahusu masuala ya mashirikiano ya kidiplomasia na uchumi na biashara baia ya nchi hizo mbili.
Alisema kuwa pamoja na mambo mengine Rais Samia na Rais wa Botswana Dr. Masisi watajadili namna ya kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa nchi ya Botswana kutokana na nchi hiyo kukubaliana kuandaa mitaala ya kufundisha lugha ya kiswahili katika vyuo vikuu pamoja na kutumia lugha hiyo katika idara za mambo ya nje ya Botswana.
Aliendelea kusema kuwa upande wa uwekezaji katika biashara Tanzania na Botswana hadi kufikia mwaka 2020 kiasi cha shilingi bilioni 3.5, mwaka 2019 ilikua shilingi bilioni 1.8, ukilinganisha na mwaka 2016 ambapo ilikua kiasi cha chini cha shilingi milioni 731 pekee.
"Botswana inafanya vizuri katika sekta ya Madini na Mifugo hivyo kupitia ziara hiyo, Rais Samia na rais Dr. Masisi watajadili namna ya kushirikiana katika sekta hizo,Tanzania kujifunza kufuga kwa kisasa, Botswana wanauza nyama duniani kote, pia ina mpango wa kuanza kuuza nyama hapa nchini kwetu,lakini hata sisi tunatarajia kuuza mazao ya bahari kama vile Dagaa "Alisema.
Akizungumzia hali ya Ugaidi iliyofanywa na vikundi vya uasi katika jimbo la Cabo Delgado lilopo karibu na mpaka wa Tanzania Balozi Mulala alisema kuwa wakuu wa nchi za SADC bado wanaendelea kukutana mjini Maputo nchini Msumbiji kwa ajili ya kujadili namna ya kukomesha ugaidi huo.
Alisema Rais Dr. Masisi wa Botswana ndiye mwanyekiti mpya wa Jumuiya hiyo hivyo kufuatia ziara hiyo atajadili na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan juu ya hali ya usalama katika nchi ya Tanzania na Msumbiji kufuatia vitendo vinavyofanywa na vikundi vya waasi katika jimbo hilo.
"Sadc inaendelea kuchukua hatua ya kutuma vikosi vyake vya ulinzi na usalama, lakini pia tumeomba umoja wa mataifa utusaidie kushirikiana nasi, manake vikundi vya waasi vimeua watu, vimesababisha uharibifu wa mali, pamoja na raia wa Msumbiji kukimbia makazi yao, kwahiyo wakuu wanchi za Sadc bado wanaendelea kuchukua hatua" alisema Balozi Mulamula
No comments