Breaking News

Kambi ya Mashindano ya Watunisha Misuli Rasmi June 8 Dar

Katika kuhakikisha sekta ya michezo inakuwa nchini shirikisho la watunisha misuli nchini (TBF) imeandaa kambi ya mashindano hayo inayotarajiwa kuanza juni 8 mwaka huu.

Kambi hiyo itakayo wajumuisha watunisha misuli wanawake na wanaume wenye uzito wajuu kuanzia kilogram 91, sambamba na wenye uzito chini ya kilogram 90.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Makamu mwenyekiti wa shilikisho hilo Crispin Mwemwe alisema mashindano ya mwaka huu yataanza Juni 8 yatajumuisha miss fitness na free weight.

"Mashindano ya mwaka huu yatajumuisha makundi manne uzito wa juu na uzito wa Kati  kwa wanaume, wakati wanawake  watajumisha makundi manne  ikiwemo watunisha misuli wa ufukweni  watunisha misuli wa ngazi ya juu wakati na wa kawaida,"Alisema Bw. Mwemwe.
Bw. Mwemwe alisema mshindi wa Kwanza wa uzito wa kilogram91 kwa wanaume anatajiwa kujizolea kitita cha shilingi milioni 5, mshindi wa pili mwenye chini ya uzito kilogramu 90 atajishindia kitita cha shilingi milioni 3, wakati mshindi wa 3 atajizolea shilingi milioni 3.
Alisema kwa upande wa mshindi wa uzito wa juu wa zaidi kilogramu 91 atapata milioni 3, Uzito wa chini kilogram 91 atapata kitita cha shilingi milioni 2, mshindi wa ngazi ya chini atapata kitita cha milioni mbili.
"Na Mshindi wachini ya uzito  wa chini VB wakilo90 atapata kitita cha shilingi milioni moja wakati chiniuzitokiogram90 atajipatia kitita cha milioni moja"Aliongeza  Mwemwe.

Baadhi ya washiriki wakionyesha nna walivyojipanga kushiriki kambi hiyo.

No comments