Kampuni ya Kansai Paint Yazindua Rangi Mpya za Kisasa
Rangi za Plascon zina ubora wa hali ya juu na zina faida zaidi ya rangi ya kawaida; 1) Plascon Anti Mosquito Paint ni rangi mpya kabisa na ni ya kwanza Tanzania yenye uwezo wa kuua mbu muda mfupi baada ya kutua ukutani
2) Rangi ya Plascon Weatherguard ni rangi namba moja ya kuzuia ukungu na fangasi kwenye jengo na inahimili mabadiliko ya hali ya hewa
3) Rangi ya Plascon Vinyl Silk inadumu muda mrefu, rahisi kusafisha kuta zako na haipauki.
4) Rangi ya Plascon Super Gloss inauwezo mkubwa wa kulinda na kufunika sehemu mbali mbali zikiwemo kuta za jengo, mbao na chuma.
Kansai Plascon wana rangi zaidi ya 5000 na zinapatikana madukani kote nchini na kwa kupitia mawakala wetu.
Kampuni ya Kansai Plascon katika kampeni yake ya PLASCON NI ZAIDI YA RANGI, imemtambulisha rasmi Msanii Lucas Mhuvile almaarufu kama Joti na Nishai kuwa balozi wa rangi za Plascon na kuwa fundi rangi namba moja Tanzania.
Kwa upande wake Nishai alisema “Ninayo furaha kubwa sana kujiunga na familia ya Plascon na kupata mafunzo ya upakaji rangi. Nitatembea nchi nzima nikitoa mafunzo na kuongea na mafundi wenzangu na wateja ili kuwadhirishia ubora wa rangi za Plascon na kuonyesha jinsi Plascon ni Zaidi ya rangi za kawaida.”
Aliongeza “Wananchi wote wanauwezo wa kupata taarifa mbalimbali kuhusu rangi za Plascon na kuzungumza moja kwa moja na mimi kupitia mitandao yangu ya kijamii, na nitazidi kutoa mafunzo na ushauri kupitia Whatsapp namba 0737 72 71 83 ili kuongeza uelewa wa utaalamu huu wa kupaka rangi kwa wananchi.”
Kuhusu Kampuni ya Kansai Paint
Makao makuu ya Kansai Paint yapo nchini Japan, na ipo kwenye orodha ya makampuni 10 makubwa zaidi ya rangi dunian na ni moja ya kampuni za rangi zinazo ongoza duniani kwa ubora wa rangi za magari na majengo. Kansai Paint ni kampuni inayoongoza kwa Ubora na Utoaji wa bidhaa zinazo kidhi mahitaji ya wananchi kwenye soko la Afrika Mashiriki.
Mawasiliano: 0713900698 or 022 2865141/2 au kutembele web yao www.kansaiplascon.co.tz au ukurasa wa mtandao ya kijamii https://www.facebook.com/PlasconTZ na https://www.instagram.com/plascontanzania/
Post Comment
No comments