Maonyesho Ya 45 Biashara Ya kimataifa Ya Dar es salaam (Sabasaba) Kuanza Juni 28
Waziri wa viwanda na biashara Kitila mkumbo ametanga kuanza rasmi kwa maonyesho ya 45 ya ya biashara sabasaba kuanzia juni 28 mpaka julay 13 ambapo ametoa wito kwa wajasirimali na wafanyabiashara kuendelea kujitokeza ili kupata fursa ya kuonyesha bidhaa zao.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo wakati akitoa taarifa hiyo amesema kuwa maonyesho ya sabasaba kila mwaka nchi 35 hushiriki lakini kutokana na janga la covid 19 zimepungua na kufikia nchi 7.
"Katika kipindi cha nyuma maonyesho ya sabasaba nchi 35 zilikuwa zikishiriki maonyesho hayo lakini kutokana na janga la covid 19 zimepungua na kufikia nchi 7 mwaka huu." Alisema Prof Mkumbo.
Alisema takribani makapuni 54 kutoka nje ya nchi zimethibisha kushiriki huku kampuni za ndani 2803 zitashiriki huku bei ya kiingilio na mabanda ikibaki ileile kwa zaidi ya miaka 10.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maendeleo ya biashara Nchini (TAN TRADE) Bw.Edwin Rutageruka alisema katika maonyesho ya mwaka huu kutakuwa na banda maalumu la watu wenye ulemavu mbalimbali ili kutoa fursa kwao kuonyesha bidhaa na bunifu zao.
Akizungumzia namna ambavyo wamejipanga katika kuhusu janga la COVID 19 alisema tayali wameaandaa kamati maalumu kwa kushirikiana na hospital mbalimbali nchini ili kuhakikisha tafadhali zote dhidi ya Covid 19 zinachukuliwa ili kuepusha kusaambaa kwa virusi hivyo.
"TANTRADE tayali umeunda kamati maalum ambayo inaundwa na wataalam kutoka taasisi mbalimbali za afya nchi pamoja na wadau kuhakikisha taadhali zote dhidi ya COVID 19 zinazingatiwa"
Post Comment
No comments