Waziri Mkuu Majaliwa Mgeni Rasmi Tamasha la Karibu Dodoma Festival
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. Kasimu Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la karibu Dodoma Festival 2020 litakalofanyia kuanzia 12 Agust mpaka 15 jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mratibu wa tamasha hilo bw. Simon Mwapangata maarufu kama (RADO), alisema tamasha hilo mahususi kwa lengo la kupongeza Rais WA jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada ambazo amekuwa akizichukua za kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi tangu aingie madarakani.
"Tamasha la karibu Dodoma Festival limejikita katika kupongeza rais Magufuli kwa hatua mambazo amekuwa akizichukua tangubaingie madarakani pamoja na kuenzi na kutimiza mawazo na maono ya Bana wa Taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere likiwemo la serikali kuamina makao makuu ya mji jijini Dodoma"
Alisema kwa kutambua mchango rais Magufuli katika kipindi kifupi cha uongozi wake tamasha hilo watamtunuku tuzo ya heshima ya uongozi uliotukuka pamoja na kutoa vyeti vya heshima kwa viongozi wa serikali.
"Kwa kutambua jitihada zake za dhati tamasha la karibu Dodoma Festival litampa Tuzo ya heshima mhe Rais sambamba na kuwapatia vyeti vya heshima maspika wote wa bunge la jamhuri ya muungano tangu tupate uhuru kutambua mchango wao kwa taifa pamoja na wasanii walio amasisha uzalendo kwa taifa" Alisema bw. Mwapangata.
Mapema akizungumzia tamasha hilo mwakilishi wa wadhamini wa tamasha hilo ambae pia ni mshauri mkuu bw. QS Mhonda alisema tamasha hilo la siku nne ni mahususi kwa wale wote wapenda maendeleo ambae anaona na kuthamini juhudi za mhe rais Magufuli katika kwalerea maendeleo wananchi.
"Sisi kama wadhamini wa tamasha hili la karibu dodoma festival tunatambua jitihada na juhudi za makusudi ambazo mhe rais Magufuli amekuwa akizichukua katika kuleta maendeleo kwa taifa hivyo kwa kutambua hilo tumeshirikiana na waratibu wa tamasha kuweza kutambua juhudi hizo" Alisema bw. Mhonda.
Tamasha la Karibu Dodoma Festival ambalo litafanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la dodoma ma kuhitimishwa katika uwanja wa Jamhuri shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo kuamasisha usafi, umoja na mshikamano, amani na upendo, maonyesho ya utamaduni, Tuzo pamoja na kuzindua wimbo wa Tanzania Yetu ni Nchi ya Kusifiwa
No comments