NEC Yatangaza Tarehe Rasmi ya Uchaguzi
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya Uchaguzi wa Rais na wabunge wa Jamhuri ya Muungano na madiwani wa Tanzania Bara.
Akizungumza leo Julai 22,2020 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (mstaafu)Semistocles Kaijage amesema kwamba katika
Ratiba hiyo uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais, ubunge na udiwani itakuwa Agosti 25 mwaka huu na kampeni za uchaguzi zitaanza Agosti 26 hadi Oktoba 27 mwaka huu.
Amesema kwa mujibu wa ratiba ya NEC siku ya Uchaguzi ni Oktoba28 mwaka huu."Tume ya Taifa kwa mamlaka iliyopewa chini ya ibara ya 41(4)ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,ikisomwa pamoja na vifungu vya 35B(1)(37)(1)(a)na 46(1)vya sheria ya Taifa ya uchaguzi.
No comments