Nyalandu Achukua Fomu, asema watahakikisha mechi wanaipeleka sawasawa, hakuna goli la kisigino
Mbowe ni mtu ambae amestahimili, amepambana na amekuwa muaminifu kwa chama hiki. Amekuwa ni kiongozi ambae ni mfano wa kuigwa na historia itamkumbuka kwamba ni mtu aliekipigania chama kuanzia ujana wake.
Usiku mmoja tulikuwa tumelala kwenye hoteli moja inayojulikana kama King David Hotel iliyoko katika mji mkuu wa Yerusalem. Mimi na Mbowe majira ya saa sita usiku tukasema tukatembelee eneo linajulikana na Waislam kama msikiti wa Suleyman na kwa wayahudi kama eneo takatifu lililojengwa na Suleyman, twende usiku wa manane na nakumbuka tulitafuta Taxi wakati huo uber hamna.
Mahali ambako kuna haki kila mtu atakuwa na amani, mfumo wa utoaji utahitaji maboresho makubwa, mwananchi yeyote anaweza akashtakiwa kwa kosa ambalo Jamhuri inaona ametenda. Mwananchi huyo bado hana hatia mpaka mahakama itakapomtia hatiani.
Kwa hiyo habari za watu amekutwa na kosa alafu anakaa keko, anakaa kizuizini mwaka wa nne, habari hizo zitakuwa ni historia ya kusikika. Hatutawaweka watu kizuizini wawe wanaCCM au wanaCHADEMA, tutataka haki na mifumo iwe sawa kwa watu wote.
Yeyote atakaeteuliwa na chama tutamuunga mkono, tunaweza tukashinda kama tutakuwa wamoja.
Tutahakikisha tunaipeleka hii mechi sawasawa, magoli tutafunga asubuhi, mchana. Hakuna goli la kisigino na niwahakikishie watanzania ambao wameingiwa na hofu, mtanzania anatembea anaona jani limedondoka anadhani nyoka anageuka. Naomba niwaambia saa ya kuondoa woga ndani ya nyoyo zetu, ndani ya nchi yetu imefika.
Hofu huua creativity, mtoto akiingiwa na hofu, maono yake yanakufa. Tuondoe hofu. Uchaguzi utakuwepo, hakuna ambae atapitishwa kwa sababu mtu mmoja amesema atapitishwe, niwahakikishia nchii hii ina mkubwa ambae anaitwa Mungu alie hai, nchi hii ina mwenyewe.
Mwanamuziki wa Kenya amesema muombee jirani yako aishi muda mrefu ili unapobarikiwa ajionee mwenyewe. Ni matamanio yangu, wakati niko CCM tulikuwa tunaimba wacha waisome namba. Hatutaki mtanzania yeyote aisome namba yoyote zaidi ya namba ya heri ya Tanzania.
CHADEMA ikichukua madaraka, ijiandae kukosolewa na wale wanaoikosoa warudi nyumbani wakalale salama kwa sababu katika kukosoana tunaandaa taifa lililo bora.
Katika mandhari mpya ya CHADEMA tukishirikiana na wengine, tutamruhusu kila mtanzania astawi tena, talanta zistawi tena, tukalijenge upya taifa ambalo alikuwa na maono nalo baba wa Taifa.
No comments