Breaking News

Naibu Katibu Mkuu ADC Atangaza Nia Kugombea Urais Zanzibar


Naibu katibu mkuu wa chama cha ADC Bi. Queen Sendiga ametangaza nafasi ya kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakaofanyika octoba 25 mwaka huu.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam alisema anayo dhamira ya dhati ya kugombea  ili kuweza kuwaletea maendeleo.

"Napenda kutangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya urais kama nitapatiwa ridhaa  na chama kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania" Alisema Bi. Sendiga 

Alisema kupitia sera na mikakati ambayo chama anayo matumaini malengo makubwa kutumikia wananchi na taifa kwa ujumla katika kuwaletea maendeleo.

Katika hatua nyingne naibu katibu huyo ametoa pongezi kwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mhe. John Magufuli kwa namna ambavyo amelishughulikia na kulitatua janga la virusi vya COVID-19 nchini na kulimaliza kabisa.

"Naomba nuchukue fursa hii kumpongeza Rais Magufuli kwa namna ambavyo aliweza kupigana na janga la ugonjwa wa COVID-19 nchini na kuweza kufanimiwa kudhibiti" alisema.

No comments