Breaking News

Mkutano Mkuu wa Chama Cha ADC kufanyika Julai 25 Zanzibar


Chama Cha siasa Cha Alliance for Democratic Change (ADC ), kinatariji kufanya mkutano mkuu visiwani
 Zanzibar Julai 25  kwa ajili ya kuwateua majina ya nafasi wagombea wa nafasi za uongozi mbalimbali ikiwemo urais ambaye atapeperusha  bendera ya chama hicho ktk uchaguzi mkuu utakaofanyia mwezi octoba.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama buguruni jijini dar es salaam Katibu Mkuu wa ADC,  Bw. Doyo Hassan Doyo alisema mkutano huo pamoja na mambo mengine utapitisha majina ya watia nia katika nafasi mbalimbali.

"Mkutano huo ambao utafanyika Julai 25 visiwani Zanzibar wajumbe wa mkutano Mkuu watapitia majina,  kuchambua na kuwateua mgombea nafasi urais Tanzania bara na Zanzibar ambae atawakilisha chama katika uchaguzi mkuu ujao" Alisema bw.Doyo

No comments