Bi QUEEN SENDIGA Achukua Fomu Kugombe Urais Kupitia Chama Cha ADC
Mwanachama wa chama cha Chama Cha siasa Cha Alliance for Democratic Change (ADC ), Bi. Queen Cuthbert Sendiga leo amechumua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tikeki ya chama hicho jijini dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo alisema ameamua kuchukua fomu kushiriki kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuonyesha kuwa wanawake wanao uwezo kushiriki na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini.
"Nimechukua fomu ya kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kuwa na kiu kubwa ya kuwatumikia watanzania katika kuwaletea maendeleo ya kweli kama nitafakiwa kupitishwa na chama changu na kuchaguliwa na watanzania"
Alisema pamoja na serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli kufanya mambo mengi mazuri katika nyanja mbalimbali bado aijafanikiwa kuyateleza kwa kiwango cha kutosha.
Bi. Sendiga aliongeza kama atapatiwa ridhaa na chama chake na kuchaguliwa na wananchi ataunda serikali ambayo kila mmoja atashiriki kikamilifu kwa misingi ya kuzingatia haki, fursa na sawa kwa wote.
"Natambua haya ni majukumu mazito na yanayohitaji mtu imara, mwenye uelewa mkubwa, jasiri, uthubutu na misimamo isiyo teteleka na zaidi yanahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuwaleta pamoja na kuwaunganisha watanzania bila kujali itikadi na tofauti zao"
Alisema chama cha ADC kimeonyesha ukomavu mkubwa na demokrasia ya hali ya juu kwa kutoa nafasi kwa kila mtu kuchukua fomu na kugombea kwa usawa hususani wanawake hivyo kuonyesha wazi kuwa wanawake wana nafasi kubwa katika chama na sio watu wa kupendelewa au kubebwa kama watu wanavyodhani.
No comments