Breaking News

Bilionea LAIZER Atembelea Banda la BRELA, Avutiwa na Utendaji Wake Ahaidi Makubwa


Bilionea wa Tanzanite, Laizer Saniniu ametembelea katika banda la Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni BRELA katika maonyesho ya sabasaba na kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na Wakala huyo nchini.

Akiwa katika banda hilo bilionea huyo aliweza kujionea na kupewa maelezo kuhusu shughuli zinazoendeshwa na kuratibiwa na wakala ambazo ni kusajili makampuni  na majina ya biashara, kusajili na kutoa leseni za viwanda,  kusimamia na kutoa hati za ubunifu, Uvumbuzi uzinduzi na uboreshwaji wa teknolojia nchini, pamoja na kuwezesha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza na kufanya biashara nchini

Akizungumza mara baada ya kupewa maelezo Bilionea huyo  alisema, amevutiwa na maelezo aliyopatiwa pamoja na huduma za Brela na kuahidi atapotaka kufungua kampuni atafuata taratibu hizo ambazo ziko kwa mujibu wa sheria.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda la BRELA katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba jijini Dar es salaam
Bilionea wa Tanzanite, Laizer Saniniu (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Baadhi ya wananchi walifika katika banda la BRELA maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika  sabasaba, kupata huduma mbalimbali.