Akili 5000 Awapongeza Wadhamini wa Club ya Yanga GSM na La liga
Shabiki na mwanachama wa Club ya Dar es Salaam Young Afrika bw. Akili Jumanne maarufu kama Akili 5000 Amepongeza hatua iliyofikiwa na Club hiyo mara baada ya kusaini mikataba miwili kati ya club na wadhamini kampuni ya GSM pamoja na La liga.
Akizungumza jijini Dar es salaam alisema hatua hiyo ya kihistoria katika vilabu vya soka hapa nchini pia ni ya kuungwa mkono na kila mwenye mpenzi mema na mshabiki wa club hiyo.
"Sisi wapenzi na mashabiki wa club ya Yanga tumeipokea hatua hiyo kwa furaha kubwa kutokana na kuona nia ya dhati ya mdhamini GSM na La Liga pamoja na Viongozi kutaka kuendesha club yetu kuwa ya kisasa zaidi" Alisema Bw. Jumanne.
Alisema kupitia mkataba huo club itakua ni moja ya vilabu bora na kuonyesha wazi kabisa nia ya dhati ya viongozi waliopo madarakani sambamba na mdamini mkuu GSM ya kutaka club hiyo kuwa moja ya club bora nchini na duniani kwa ujumla.
"Napenda kuchukua nafasi hii kutoa rai kwa wanachama na wapenzi wa club ya Yangu kutoa ushirikiano wa hali ya juu kipindi hichi amabacho club ikiwa katika mchakato wa kuelekea katika mabadiliko ya kiutendaji".
Katika hatua nyingine shabiki huyo ametoa pongezi za dhati kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli kwa hatua ambazo amekuwa akizichukua kupambana na ja ga la virusi vya COVID-19 nchini.
"Kwa dhati kabisa nampongeza mhe Rais kwa hatua ambazo ekua akizichukua katika kupambana na maambukizi ya virusi vya COVID-19 nchini jambo ambalo tunashuhudi kwasasa kuweza kuruhusiwa kuanza tena kwa michezo nchini" Alisema Akili 5000.
Pia katika hatua nyingine shabiki huyo amewapongeza viongozi wa club hiyo kwa kusimamia vizuri mchakato huo wenye tija kwa club pamoja na mashabiki katika kipindi chote club ilikuwa katika mchakato.
Pia amebainisha kuwa wanachama wa club hiyo awatakuwa tayali na kumvumilia kiongozi yeyote au kikundi chochote ambacho kitaonyesha kutaka kukwamisha mchakato huo wa mabadiliko katika club.
Post Comment
No comments