Breaking News

Wabunifu na Wanamitindo Watoa Msaada wa Vifaa Kwa Serikali Mapambano Dhidi ya maambukizi Covid-19


Wanachama wa Fashion Association of Tanzania (FAT) wameunga mkono juhudi za serikali kupambana na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na kirusi cha Corona kwa kuchangia vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Milioni 2.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti FAT Bwana Mustafa Hassanali alisema mtandao wa wabunifu nchini kwa kutambua jitihada ambazo serikali imekuwa ikizichukua kupambana na janga hili la Corona nchi wameamua kuunga juhudi hizo kwa kutoa vifaa mbalimbali ambavyo vitasaidia katika kupambana na maambukizi hayo nchini.

"Wanachama wa Fashion Association of Tanzania pamoja na wadau wengine 66 wa tasnia mitindo nchini kwa kutambua jitihada ambazo Serikali kupambana na janga la COVID-19 nchini kwa kuchingia vifaa mbalimbali ambavyo vitasaidia katika mapambano" Alisema Bwana  Hassanali.
Amevitaja vifaa ambavyo vimekabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Bi. Angelina Ngalula ni katoni 80 za vitakasa, katoni 60 kati ya hizo zikiwa ni “lit lavender disinfectant” 20 zikiwa ni “zap bleach regular".

Bwana  Hassanali ameishukuru serikali kupitia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano hususani katika kipindi hiki pamoja kuwapongeza wabunifu, wanamitindo na wadau wote wenye mapenzi mema na Tanzania kwa michango na kujitoa kwao katika kuhakikisha upatikanaji wa vitakasa hivyo kama sehemu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na kirusi cha Corona (Covid – 19). 

Aidha wabinifu hao wamwahidi  waziri kuendelea kusaidia kutoa elimu kwa Watanzania kulichukulia kwa uzito swala hilo kwani ni hatari endapo hatua stahiki hazitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufwata ushauri unaotolewa na watalaam wa afya juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa huu.

No comments