FMJ Hardware Ltd Kufanya Mnada Mkubwa wa Vifaa Vya Ujenzi Kidijitali Jijini Dar
Kampuni ya Uuzaji wa vifaa vya Ujenzi FMJ Hardware Ltd imeandaa mnada mkubwa (Promotion) kwa wateja wake ambao ambao utafanyika kidijitali (Online tv) siku ya tarehe 30 mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya kampuni hiyo Buguruni kisiwani jijini Dar es salaam, Meneja mauzo wa FMJ ltd Bw. Fredrick Sanga alisema kwa kutambua uwepo wa mlipuko wa virus vya COVID-19 nchini na hatua ambazo serikali imekua kukabiriana na janga hivyo kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano pamoja na kuwapunguzia mzigo wananchi.
"Lengo kubwa la mnada huu (Promotion) ni kuunga mkono kauli ya mhe. Rais John Pombe Magufuli kutaka tuendelee kuchapa kazi huku tukichukua taadhali juu ya ugonjwa huu wa COVID-19 sambamba na kuwawezesha wateja wetu papote nchini kuweza kununua bidhaa zetu zilizo na ubora wa hali ya juu LIVE" Alisema Bw. Sanga.
Alisema mnada huo ambao utawezesha wananchi kuweza kujipatia vifaa mbalimbali vya Ujenzi vyenye ubora na kwa gharama nafuu katika kipindi hichi cha mapambano ya CORONA nchini.
"Natoa wito kwa wateja wetu na wananchi kushiriki mnada huo ambao utakuwa LIVE kupitia Darmpya TV, Global Tv, Ayoo Tv, Icon Tv na Harakati za Jiji Tv siku ya tarehe 30 kuanzia saa 9 alasiri" Alisema
Aidha bw. Sanga ameongeza kuwa kampuni imejidhatiti kutoa huduma kwa wateja kupitia mtandao yake ya kijamaii Facebook, Instagram masaa 24 au kupiga simu namba 0653 312 438, 0716 902 995, 0717 478 770.
No comments