Tamko La Asasi Za Kiraia Kuhusu Muswada Wa Mabadiliko Ya Sheria Ya Asasi Za Kiraia Nchini
Mratibu wa Kitaifa
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Bw.Onesmo
Olengurumwa akiongea na waadau mbalimbali walioweza kuhudhulia katika mkutano
wa dharura ulioandaliwa na Asasi za Kiraia Jijini Dar es Salaam leo.
Dar es salaam:
Asasi za Kiraia
wamekutana kwa pamoja kujadili mswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali
zinazoongoza Asasi hizo na kutoa tamko lao kwa Bunge na Serikali kurekebisha
baadhi ya vifungu ambavyo kama Muswada huo utapita kutakuwa na mazingira magumu
ya utendaji kazi wa Asasi za Kiraia ikiwemo kufutwa kwa baadhi ya Asasi nchini.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Tanzania (THRDC), Bw.Onesmo Olengurumwa alisema kuwa Mei 30 mwaka huu serilaki
iliwasilisha Muswada kwa hati ya dharula wa Mabadiliko ya Sheria mbalimbali ambao
umezua sintofahamu na taharuki kwa AZAKI za ndani na nje ya nchi na huenda
lengo lilikuwa kutokushirikisha AZAKi ambao ni walengwa wakuu kwenye Muswada
huo.
“Tarehe 21 na 22
mwezi Juni mwaka huu baadhi ya AZAKi ziliweza kuwasilisha mbele ya kamati za
Bunge mjini Dodoma, Leo pia tumekutana hapa kwa dharura ili kujadili
mapendekezo yetu na pamoja na kutoa taarifa kwa umma juu ya Muswada huu, kutokana
na Umma kupaswa kujua athari za Muswada huu sio kwamba utaathiri AZAKi pekee bali
kila mtu ataathirika kutokana na kuwa AZAKi zipo kutoa huduma za kijamii, kuleta
maendeleo na ajira katika nyanja mbalimbali”. Alisema Bw.Olengurumwa.
Alisema kutokana na
uchambuzi wa awali uliofanywa na Asasi za Kiraia zaidi ya 300 kuhusu Muswada
huo walibaini kuwa ikiwa Muswada utapita kama ilivyo sasa utaleta changamoto
nyingi kwa AZAKI hasa katika utekelezaji
wake na uendeshaji wa AZAKi nchini.
Nae Mkurugenzi wa
Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Bw. Ismail Suleimani
alisema mara baada ya kupitia Muswada huo wamegundua kuwepo na changamoto na
madhara mengi yatatokea endapo Muswada huo utapita.
“Muswada huu
ukipita AZAKi zote zilizosajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni ambayo
hayakuomba Hati ya kukubaliwa kufanya kazi kama mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali ya mwaka 2002 yatatakiwa kufanya kazi kama makampuni ya kibiashara
kwa mujibu wa sheria ya makampuni na iwapo yatashindwa kufanya hivyo ndani ya
muda wa miezi miwili yatafutiwa usajili bila ya kupewa taarifa”. Alisema Bw.
Suleiman.
Wadau mbalimbali wakiwa wanafuatilia mjadala
katika mkutano wa dharura ulioandaliwa na Asasi za Kiraia Jijini Dar es Salaam.
No comments