Uzinduzi Wa Kitabu Cha Wajibu Wa Mtanzania Na Uongozi Wa Rais Magufuli Wafana Jijini Dar.
Vijana wametakiwa kujikita zaidi kujifunza na kutambua mazuri yaliyofanywa na wahasisi wa taifa letu kwa kujiandaa kuviendeleza na kuvienzi kwa faida ya vizazi vijavyo.
Akizungumza jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Wajibu wa Mtanzania na Uongozi wa rais Magufuli, kwa niaba ya Naibu waziri Juliana Shonza naibu katibu mkuu wa baraza la Kiswahili (BAKITA), Dkt. Selemani Sewangi Alisema alichofanya mwandishi wa kitabu hicho ni jambo la kuungwa mkono kutokana na cha kwanza kutumia lugha ya kiswahili.
"Kitendo kilichofanywa na mwandishi wa kitabu hiki Debora ni mfano wa kuigwa na vijana kwa kitendo chake cha kuamua kuandika kitabu ambacho kinatoa mchango na mrejesho kwa jamii juu ya mambo yaliyotekelezwa na serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na rais Magufuli tena kwa kiswahili fasaha ni jambo la kuungwa mkono."Alisema dkt Sewangi.
Alisema vijana wanatakiwa kuacha woga kutokana na rais tulienae sasa ambae ameonyesha dhamira ya dhati kwa hatua ambazo amekuwa akizichukua kuleta maendeleo kwa taifa ivyo vijana wanatakiwa kutoa mchango wao katika kufanikisha dhamira ya rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Mapemaa akizungumza wakati alimkaribisha mgeni rasmi mtunzi wa kitabu cha Wajibu wa Mtanzania na Uongozi wa rais Magufuli bi. Debora Kiyunga alisema kama kijana aliona anao wajibu wa kutoa mchango kwa jamii juu ya mambo mazuri ambayo yamefanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt John Pombe Magufuli.

"Kama kijana niliona taifa linahitaji kupata mrejesho wa hatua na maendeleo ambayo yamekuwa yakifanyika kupitia serikali ya awamu ya tano ndipo wazo la kuandika kitabu likaja" Alisema Bi Debora
Alisema kwa kutambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili nlichagua kutumia hugha hii hili iwe fursa katokana na kuwa ndio moja ya njia sahihi ya kuweza kupeleka mrejesho kwa jamii ambao utaweza kutumika vizazazi na vizazazi.
No comments