Serikali Kuendelea Kushirikiana Na Wadau Kutokomeza Ukatili wa kijinsia
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhU-dOXdGOrd4fTHEHU2coMDSXjAVC3Z862ioI-WTTZYUbkTVqKT-wo7UYQzm07hdxzkDhargvdLyAs0BZAYAKDP2797MmSzME9To9zHiG4ho4vbyJxgLVGIghRCU22H-RflgeXvtBFHH7r/s640/Screenshot_20190215-012113%257E2.png)
Serikali imesema inatambua mchango mkubwa wa wadau na taasisi zisizo za kiserikali katika jitihada za kutomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto nchini.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa kituo cha huduma (One Stop Centre) jijini Dar es Salaam Katibu MKuu wa Wizara ya Afya, Maedeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. John Jingu alisema pamoja n jitihada ambazo zimekuwa zilichukuliwa na serikali kwa kushirikia na wadau lakini takwimu zimekuwa zikionyesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimekuwa vikiongezeka kwa kasi duniani.
“Ukatili dhidi ya wanawake na watoto bado ni tatizo kubwa na halikubaliki, serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kituo hicho kinapata kila hitaji ili kiweze kutoa huduma kwa ufanisi.alisema" Alisema Dk. Jingu
Alisema kutokana na hali hiyo serikali imekuwa ikifanya jitihada mbali mbali kwa kushirikiana na wadau ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uanzishwaji wa vituo hivyo ili kuhakikisha tatizo hilo linakomeshwa nchini

![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6JWkxuhl1hDldWCn4Mm1kFRFAuNHX_fFA5bbLW2QtpDvGiTokYii9Lvz7dhrW9mpBuE0yXQGIWrJKPNgbMK6NzTLle8Td-aESAohCi3BTwReMVo1HigFVIAi5IeBRva-dBasrJ0EolSsX/s640/7-560x420.jpg)
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa CDF Koshuma Mtengeti, alisema lengo la Kituo hiki ni Kutoa huduma kwa wahanga wa kesi za ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini na wengineo wote ambao wanakutwa na ukatili wa kijinsia,
“Hili kituo hiki kiweze kujiendesha kwa ufanisi zaidi tunaiomba serikali kutenga wataalamu wa kutosha katika kuendesha vituo hivi, kutokana na kuwa takwimu ambazo zinatoka katika vituo hivi ni muhimu kuzipata kwani zitasaidia katika kupanga mipango ya baadae ya jinsi gani ya kukabiliana na tatizo hili,” Alisema bw. Mtengeti.
Alisema kituo kitatoa huduma za kisheria, ushauri nasaha, huduma ya afya pamoja na huduma ya polisi ambao watakuwa wakitoa fomu namba tatu (3) kwa ajili ya matibabu.
Aidha bw Mtengeti aliongeza kuwa hadi sasa wamekwisha toa mafunzo kwa maafisa 30 ambao watashiriki katika kuendesha kituo hicho pamoja na kufanya mazungumzo na haspitali ya Mwananyamala ili kuona ni jinsi gani ya kushirikiana kwa ajili ya kituo hicho kutoa huduma kwa ufanisi.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_H0kZiIDiqo_eT0GLQraYZ-_aMcGs0OkyzTRCz1Lc_841_I4bRdNkyYJz_J7sOd7o_N3fM62CkOZ0DM-mYBSdx3O6_bCSAqFiK6CARtIyZIp4rnWVtW5y8z2OqGEHJ1yjCivXfK8sKJzI/s640/IMG_20190214_133838.jpg)
Kwa upande wake Afisa Utumishi na Utawala wa Hospitali hiyo Mansour Karama, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu alisema wamekuwa wakipokea kwa wingi kesi za ukatili wa kijinsia zinazokumba wanawake, watoto na wanaume.
Karama alisema, kwa wastani wa kesi wanazopokea, asilimia 86 ni ukatili kwa wanawake na asilimia 14 wanaume huku aina za ukatili huo zikiwa asilimia 76 wakingono na asilimia 24 ni wakukataliwa kimwili, kijinsia na kutelekezwa.
Alisema kuwa pamoja na kupokea wahanga hao changamoto kubwa imekuwa ni vitendea kazi pamoja na wahanga kukosa pa kusemea tatizo hilo na kwamba wamekuwa wakiishia kuwapatia matibabu tu. Hivyo alishukuru kukabidhiwa kwa kituo hicho kwani kitakuwa msaada mkubwa katika kutokomeza tatizo hilo.
Mradi huo umeratibiwa na CDF kupitia ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), na kushirikana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEimv2T0CtZ7aS_MTz9LCXLxtRsJoKZSZ-hFaO15UoCSxQLWqsu5rTq69AmNy29JavCd6dnQ-cVKOVVwVQYffR1vV3ZbAbOl1709Nr_w80ZUoh58jrJ9dPIQBiEN_wd5FzoGYGjNqqU4vpFF/s640/Screenshot_20190215-011605%257E2.png)
No comments