Breaking News

Wafanyakazi Mkoa Dar Waandamana Kumpongeza Rais Magufuli

Wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuyafanya kazi kwa bidii kwa kufuata sheria na taratibu, kwa kila Halmashauri ya Wilaya pamoja na kuwatumikie wananchi vizuri kwa lugha za upole na ustaarabu.

Hayo yameelezwa Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwenye maandamano ya kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kurudisha kikokoteo cha zamani cha mafao kwa wafanyakazi wa Serikali.

DC. Lyaniva amesema kuwa jambo la furaha kubwa alilolifanya Rais Magufuli anastahiki apongezwe na kila mtu kwani ameonyesha uzalendo mkubwa kukifuta kikokotoo kipya kwani kilikua kinaenda kuwakandamiza wafanyakazi.

Aidha ameongeza kuwa wanampongeza sana Rais Magufuli amefanya mambo mengi makubwa kwa wananchi ikiwemo kuboresha miundombinu kujenga madaraja, ujenzi wa njia nane pamoja barabara lengo ni kuoana wananchi wake wanaishi mazingira mazuri

“Amefanya makubwa sana Rais wetu Magufuli amepambana na rushwa na ufisadi, amefanikiwa kwa kiwango kikubwa ameziba mianya yote anawapenda sana walimu amefanya maboresha maeneo mengi kusudi wafanye kazi katika mazingira mazuri” Amesema Lyaniva.

Hata hivyo amesema haya anayoyafanya Rais Magufuli yanahitaji pongeza sana kwani ametoa matibabu bure kwa wazee, elimu bure kwa wanafunzi, huo ndio uzalendo kama walionao waandishi wa habari katika kuuhabarisha umma hivyo kuwe na nidhamu ya kazi.


No comments