Breaking News

Musiba:Na Taarifa Za Kuwepo Njama Za Kumchafua Rais Magufuli Na Serikali Yake Kupitia Tundu Lissu.

Mwanaharakati uhuru na mkurugenzi wa kampuni ya CZI, Bw Cyprian Musiba amesema anazo taarifa za kuwepo kwa mpango wa Kumchafua rais magufuli pamoja na serikali yake ambao umeratibiwa na vigogo wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema kupitia Mhe. tundu Lissu. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam alisema mpango huo ambao uratibu umeshakamilika na waraka husika tayali alishapelekewa mhe Lissu ili kuanza kusambaza katika mataifa ya nje pamoja na kupitia vyombo vya habari vya Magharibi na vya ndani atakapolejea nchini. 

"Ninazo taarifa kuwepo na mpango wa Kumchafua Rais Magufuli na serikali yake ndani na nje ya nchi mpango ambao umeratibiwa na tayali umeshakabidhiwa kwa Mhe Lissu kuweza kusambaza katika mataifa ya magharibi na mara baada ya kurudi nyumbani" Alisema bw Musiba.

Alisema mpango huo ambao umelenga kutumia tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa mbunge huyo mjini Dodoma na watu wasiojulikana pamoja na mambo mengine ambayo wamekuwa wakiyataja kama uhuru wa kujieleza pamoja na muswada wa vyama vya siasa.

Nitoe rai kwa Mhe lissu kuachana na mpango huo kwani auna tija kwa taifa badala yake ajikite katika kumsaidia rais Magufuli kwa rais magufuli ni rais ambaye amechaguliwa na watanzania ivyo kitendo cha kutaka kumwujumu kunaweza kuhatarisha amani sambamba na kutoheshimu maamuzi ya watanzania.

"Mhe lissu aangalie taifa kama Libya lilikuwa ni moja ya mataifa bora kabisa lakini kutokana na kuwepo machafuko katika taifa hilo hivyo kushindwa kuwa na amani kama iliyokuwepo awali." Alisema

Aidha bw. Musiba amewapa onyo watu ambao wamekuwa  wakiliujumu gazeti lake la Tanzanite kwa kuchapisha habari za uongo na kusambaza katika mitandao ya kijamii kuacha mara moja. 

No comments